**********
NJOMBE
Familia moja ya Mathias Mgaya yenye makazi yake katika kijiji cha Kipengele kata ya Kipengele wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe imeomba serikali kuipa ulinzi wa ziada baada ya kuwapoteza ndugu wawili wa familia moja ambao wamedaiwa kuuwawa na wakazi wa kijiji hicho.
Familia hiyo imelazimika kuomba ulinzi kutokana na vitisho vya mara kwa mara ambavyo imekuwa ikivipata kutoka kwa watuhumiwa ambao walisha fungwa na kuachwa huru kwa kesi za mauaji.
Anitha Seveyage ambaye ni mama mzazi wa marehemu hao wawili ambao ni Huruma Mgaya na Eliah Mgayana Benadetha Mgaya ambaye ni mdogo wa marehemu hao wamesema tangu watuhumiwa hao wanne watoke gerezani baada ya kukaa mahabusu miaka miwili kwa tuhuma za mauaji , wamekuwa wakiwapa vitisho kwenye familia yao jambo ambalo linahatarisha maisha yao na kuiomba serikali kuwapa ulinzi kunusuru maisha yao.
Wakizungumzia kuhusu matukio hayo kwa nyakati tofauti viongozi wa kijiji akiwmo Otimali Mwinuka ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Kipengele na Beatus Msovela afisa mtendaji wa kijiji wanakiri kutokea kwa mauaji hayo pamoja na vitisho kutolewa kwa viongozi na wanafamilia jambo ambalo limezidi kuhatarisha usalama na amani kijijini hapo.
Kutoka mahabusu kwa watuhumiwa wa mauaji kuna muibua mke wa Huruma Mgaya bi Ajentina Sigala ambaye anasema kifo cha mme wake kimemuacha kwenye wakati mgumu na kwamba anamuachia mungu kutoa majibu ya haki ya mmewe.
Kufuatia malalamiko hayo mtandao huoo umelazimika kufika katika ofisi ya Taifa ya Mashitaka na kuzungumza na mwanasheria wa serikali mkoa wa Njombe Yahaya Misango ambaye ameongea kwa sharti la kutorekodiwa ambaye anakiri kwamba ofisi yake ilipokea faili namba 8 la mwaka 2019 la shauri la washtakiwa, lakini baadae walilifuta faili kwa kuwa hakukuwa na kesi ya msingi na ushaidi uliojitosheleza na kutoa ushauri kwa walalamikaji kwamba wanaweza kurudisha shauri hilo kama ushahidi ukikamilika.