TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Pwani, imebaini mapungufu kwenye miradi ya maendeleo mitatu yenye thamani ya sh.bilioni 800.
Aidha imefanikiwa kuongeza mapato kwenye Halmashauri ya Chalinze kutoka milioni 300 hadi milioni 600 kwa mwezi baada ya kufanya udhibiti ambapo ni sawa na bilioni 3.6 kwa mwaka.
Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani Suzana Raymond alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa miradi hiyo ni kwenye sekta ya elimu, afya na maji.
Raymond alisema ,katika kipindi kipindi cha April juni jumla miradi 36 yote thamani bilioni 11 kati ya hiyo 3 thamani bilioni 800 ina mapungufu .
“Pamoja na majukumu mengine TAKUKURU inafanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri za mkoa wa Pwani kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa na kuzingatia thamani ya fedha Value for Money,” alisema Raymond.
Akizungumzia kuhusu kuokoa fedha kwenye Halmashauri ya Chalinze alisema kuwa walifuatilia mfumo wa ukusanyaji wa mapato katika machimbo ya kokoto Lugoba na kubaini mapungufu ya upotevu wa mapato.
Alibainisha kutokuwepo kwa watumishi wa halmashauri kwenye mageti,kutokuwepo na utaratibu mzuri wa vitabu vya ukusanyaji wa mapato,kuchezea mashine za pos,kutokuwa na wakala wa mizani kwenye machimbo ya kokoto, kutokuwa na idadi kamili ya makrasha.
Baada ya kubaini mapungufu takukuru wilaya na mkuu wa wilaya Bagamoyo na wadau na kuweka mikakati ya kuziba mianya hiyo na matokeo ya utekelezaji wa maazimio hayo umesababisha ongezeko la mapato kutoka milioni 300 hadi milioni 600,”alisema Raymond.
Alisema kuwa katika kipindi hicho ofisi ilipokea malalamiko 159 sawa na ongezeko la asilimia 62.3 kati ya hayo malalamiko 71 yanahusiana na vitendo vya rushwa na uchunguzi wake unaendelea na mengine uchunguzi ulikamilika na watuhumiwa kufikishwa mahakamani.
“Malalamiko 88 hayahusiani na vitendo vya rushwa na wahusika na wengine walisaidiwa kwa kuwasiliana na idara husika kwa lengo la kutatuliwa kero zao na idara zilizolalamikiwa zaidi ni Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) malalamiko 51, mahakama 21, polisi malalamiko 15 na mengine yaliangukia idara zingine kwa idadi ndogo,” alisema Raymond.
Aidha alisema kuwa katika kipindi cha Aprili – Juni chambuzi za mifumo 13 zilifanyika ili kubaini mianya ya rushwa na maeneo yaliyofanyiwa uchambuzi huo ni kwenye ukusanayaji wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu, miradi ya maji, miradi ya matrekta, mfumo wa manunuzi kwa kutumia nguvu za wananchi, utoaji wa mikopo ya wanawake na vijana na ukusanyaji wa mapato.
“Tumeendelea kutoa elimu kwa umma kwa kutumia mbinu mbalimbali za uelimishaji ambapo zilifanyika semina 15, mikutano 42, klabu za wapinga rushwa 83 zimefunguliwa na kuimarishwa na makala 12 ziliandaliwa hivyo uelimishaji huo umewafikia jumla ya wananchi 7,006,” alisema Raymond.