Baadhi ya Madiwani wakifuatilia jana taarifa ya Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) Erasto Juma wakati wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Igunga la kujadili hoja mbalimbali za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.
Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) Erasto Juma akiwasilisha taarifa jana wakati wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya igunga la kujadili hoja mbalimbali za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.
*************
NA TIGANYA VINCENT
TABORA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Igunga inatarajia kuchukua hatua za kisheria kwa ikiwemo kuvikisha Mahakamani vikundi vya wanawake na vijana ambavyo havijarejesha mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 144.2.
Majibu hayo yalitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Revocatus Kuuli wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Nje .
Alisema Mwanasheria ameshaanza utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani wadaiwa wote ambao hawajafanya marejesho ya mikopo waliopatiwa na Halmashauri.
Awali akiwasilisha taarifa kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mku wa Hesabu za serikali (CAG) kuhusu ukaguzi ulifanyika Igunga Mkaguzi wa Nje Erasto Juma alisema kiasi cha milioni 21 kati ya shilingi milioni 165.3 kimehakikiwa.
Alisema mikopo ambayo haijarejeshwa inapaswa kurejeshwa na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga inapaswa kutotoa mikopo kwa vikundi ambavyo havitekelezi mikataba.
Juma aliongeza kuwa Halmashauri hiyo inapaswa kuchukua hatua stahiki kwa wale wote wambao hawajaresha mikopo iwemo za ya kisheria.
Kwa upande wa Madiwani waliunga mkono wahusika kuchukuliwa hatua ikiwemo kuwafikisha Mahakamani ili waweze kurejesha fedha kwa ajili ya kupata fedha za kukopesha vikundi vingine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey alisema kuwa ni vema hatua za kisheria zikachukuliwa kwa wadaiwa wote ili fedha zilizotolewa zirejeshwe kwa ajili ya kutoa kwa vikundi vingine na ziweza kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) Erasto Juma ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kuhakikisha maeneo yote ya wazi wanayomiliki yanapimwa na kuwa na hati miliki.