Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine alipowasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Mwashambwa, mara baada ya kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sifuni Msangi, mara baada ya kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi (mbele katikati) akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine (mwenye tai), kuangalia eneo lililotolewa kwa SMZ kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi zake Mahona Makulu jijini Dodoma.
Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe (kushoto) akitoa maelezo kuhusu eneo lililotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
…………………….
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi ameoneshwa na kutembelea eneo ambalo zitajengwa Ofisi za Serikali hiyo eneo la Mahoma Makulu Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Balozi Iddi ambaye aliambatana na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali, alishukuru Serikali kwa kupewa eneo hilo.
Aliahidi kuwa SMZ itaaaza ujenzi wa Ofisi zake katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kama watapata fungu ujenzi utaanza mapema iwezekanavyo ili waweze kuhamia katika Makamo Makuu ya Nchi.
Katika ziara hiyo ujumbe huo kutoka Zanzibar ulipokelewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi, Samuel Mwashambwa hiyo na viongozi mbalimbali
Balozi Seif alipata nafasi ya kutembelea pia eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba ambako zimejengwa Ofisi 25 za Serikali zikiwemo za Wizara mbalimbali na tayari watumishi wake wamehamia.
Akizungumza kuhusu eneo hilo Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe alisema eneo hilo lina ekari 30.
Alisema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza Serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi Julai 25, 2016 ulianzishwa mchakato wa kuhamisha watumishi.