Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja MWAKILA S/O ALLY [32], mkazi wa Mwambene, Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu [141] zenye usajili wa majina ya watu wengine.
Mnamo tarehe 12/07/2019 majira ya saa 13:00 mchana huko mtaa wa Itongo kata ya Mwambete tarafa ya Iyunga. Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi umeme baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo za simu 141 za mitandao tofauti zilizosajiliwa kwa majina tofauti ikiwemo “HALOTEL” laini 13, TIGO laini 29, TTCL laini 01, VODACOM laini 78 na AIRTEL laini 20. Pia alikutwa akiwa na vocha zilizotumika za Vodacom 05, Tigo 04, Airtel 48, Halotel 03 pamoja na simu Itel 03, “Oking” 01 na “Hotwave” 01.
Chanzo ni kujipatia kipato. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja MWAKILA S/O ALLY [32], mkazi wa Mwambene, Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu [141] zenye usajili wa majina ya watu wengine.Mnamo tarehe 12/07/2019 majira ya saa 13:00 mchana huko mtaa wa Itongo kata ya Mwambete tarafa ya Iyunga. Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi umeme baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo za simu 141 za mitandao tofauti zilizosajiliwa kwa majina tofauti ikiwemo “HALOTEL” laini 13, TIGO laini 29, TTCL laini 01, VODACOM laini 78 na AIRTEL laini 20. Pia alikutwa akiwa na vocha zilizotumika za Vodacom 05, Tigo 04, Airtel 48, Halotel 03 pamoja na simu Itel 03, “Oking” 01 na “Hotwave” 01.Chanzo ni kujipatia kipato. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Imetolewa na:[ULRICH O. MATEI – SACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.