Watoto wakiwa mkao wa kula ikiwa ni sehemu ya vionjo vya ngoma ya Wamakua inayochezwa msimu wa mavuno.
Afisa elimu wilaya ya Mbozi Hosana Nshullo akiwasilisha hali ya sekta ya elimu mbele ya wadau wa elimu wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Halima Mpita akizungumzia mkakati wa ujenzi wa mabweni kwaajili ya kuwaweka kambini vijana wenye vipaji vya michezo mashuleni
Watoto wa shule ya Msingi Isangu wakionyesha ujuzi wa kucheza ngoma ya jamii ya wamakua inayochezwa kwenye mavuno, ikiwa ni sehemu ya kupamba mkutano huo ulioambatana na kuutangaza mfuko wa elimu wilaya ya Mbozi ili kukusanya michango kwaajili ya uendelezaji miundombinu ya elimu
**************
Na Danny Tweve -Mbozi
Wilaya ya Mbozi imo kwenye mkakati wa kuanzisha mabweni kwaajili ya watoto wenye vipaji vya michezo kwenye baadhi ya shule za kata ili kuwezesha watoto hao kuendelea kukuza vipaji vyao kambini kutokana na wilaya hiyo kuendelea kufanya vyema kwenye eneo la michezo
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa elimu wilayani humo, Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Mbozi Bi Halima Mpita amesema tayari wameanza mkakati huo kwenye shule zake baada ya kupata wadau wa kuchangia ujenzi huo.
Halima Mpita ni miongoni mwa watanzania waliothibitishwa na wizara ya elimu na ufundi kwenye eneo la Ubunifu akiwa miongoni mwa watanzania 18 waliobainishwa kwenye shindani mbalimbali za ubunifu.
Amesema hatua hiyo itawezesha vipaji vinavyoibuliwa mashuleni kukuzwa na kwamba katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo wilaya hiyo na mkoa wa Songwe kwa ujumla imekuwa miongoni mwa mikoa inayowakilisha vyema kwenye mashindano ya michezo ya UMISETA (kwa shule za sekondari) na UMITASHUMTA (kwa shule za msingi) .
Katika hatua nyingine kikundi cha ngoma cha shule ya Msingi Isangu kiliweza kuwanyanyua watu waliohudhulia mkutano huo kutokana na burudani yake ya ngoma ya jamii ya Wamakua kutoka mkoa wa Mtwara ambapo wengi walishindwa kujizuia na kuwatuza watoto hao.
Mwanariadha wa zamani marehemu Erasto Zambi ni miongoni mwa wanariadha waliowika miaka ya nyuma kwa kufukuza upepo ni sehemu ya matunda ya wilaya ya Mbozi. mwingine katika mchezo wa riadha ni Zaina Mwashambwa.