*************
NJOMBE
Wawekezaji wilayani Njombe wamesema licha ya rais kuagiza watalaamu wa ngazi mbalimbali serikali kuondoa vikwazo visivyo na tija kwa wawekezaji wenye uhitaji wa kujenga viwanda , imedaiwa bado wameendelea kukabiliwa na tatizo hilo na kukwamisha jitihada zao za kuendeleza uchumi wa viwanda.
Hayo yamebainishwa na wawekezaji wa viwanda vya kusindika unga katika halmashauri ya mji wa Njombe walipokutanishwa na mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edwad Mwalongo kwa lengo la kujadili changamoto katika biashara hiyo pamoja na kuweka mikakati ya kulifikia soko la mahindi katika nchi ya Congo ambako kunatajwa kuwa na puhitaji mkubwa wa mazao ya chakula .
Salum Sanga na Clemence Malekela ni baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji katika sekta ya viwanda vya kuchakata unga ambao wanasema bado wameendelea kukabiliwa na changamoto ya watalaamu wa halmashauri kugoma kutoa vibali vya kujenga viwanda pamoja na maeneo tengwa ya viwanda.
Wakizungumzia kuhusu soko wawekezaji hao wa ndani ya mkoa wa Njombe wanakiri kwamba zaidi ya miaka mitatu wakulima wameshindwa kuuza mahindi kutokana na kuporomoka kwa soko na kwamba kitendo cha mbunge huyo kwa kushirikiana na serikali kufungua masoko ya nje ya nchi kama Zambia , Kenya na Congo itasaidia kukata kiu yao.
Wakati mbunge wa Njombe mjini Edwad Mwalongo akieleza shauku yake ya kupambana kulitafuta soko la mahindi nje ya nchi lakini pia amewataka wakulima na wawekezaji hao wa viwanda vya unga kuto sita kukopa mashine na fedha katika benki ya kilimo TADB ambayo imeamua kumkwamua mkulima kwa kumkopesha mashine za kisasa za kuchakata mahindi pamoja na mikopo ya maghara yenye tani 500.