Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mhe.Mwita Waitara, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,akitoa taarifa wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,akitoa ripoti ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika hilowakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kutoka UNFPA,Bw.Samwel Msokwa, akisoma taarifa ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wakifuatilia maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara, akizindua Ripoti ya Idadi ya watu Duniani,kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,wa pili ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi na kulia ni Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara,akiwa katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya kuzindua Ripoti ya Idadi ya watu Duniani,Kulia ni Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi wakiwa wameshika ripoti hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara,akiwa amenyanyua vitabu mara baada ya kuzindua Ripoti ya Idadi ya watu Duniani,uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………
Na Alex Sonna, Dodoma.
LICHA ya Serikali kuweka adhabu kali dhidi ya watu wanaowasababishia ujauzito wanafunzi na watoto waliochini ya umri wa miaka 18, lakini bado tatizo la mimba za utotoni ni kubwa huku mila na desturi zikitajwa kuchangia tatizo hilo hapa nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara, wakati maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Mhe. Waitara amesema tatizo hilo ni kubwa kwa shule za msingi na sekondari ambapo ni asilimia 29 na linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mila na desturi, uendeshaji wa kesi ya kumtia mtu hatiani aliyempa mimba wanafunzi.
“Kuna mila na desturi ambazo watoto wa kike wakifikia umri fulani wanapewa chumba hivyo huko mtaani usiku kucha huwezi jua kinachoendelea, mazingira magumu ya usomaji.
“Hata katika uendeshaji kesi hizi mpaka kumtia mtu hatiani bado ni changamoto sana kwa kuwa wanaofanya vitendo hivyo wengine ni watu wa karibu na familia na wengine wanarubuni ndugu na kumalizana kimya kimya,”amesema Waitara.
Aidha licha ya hayo amesema uelewa wa watoto bado ni mdogo huku mimba nyingi zinaripotiwa lakini zinaishia hewani bila kujua mwisho wa kesi hiyo.
Amesema wao kama serikali wanafanya vikao na wazazi mara kwa mara ili kuondokana na tatizo hili, lakini bado mwitikio ni mdogo sana katika kudhibiti vitendo hivi.
Kadhalika, amesema bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi ambapo kati ya vizazi hai 100,000 watu 556 huripotiwa kufariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utoto.
“Nchi yetu ni moja ya mataifa 179 yaliyokutana nchini Cairo na tulikubaliana kutekeleza Mpango kazi tuliopanga wa katika Mkutano huo wa Idadi ya watu na maendeleo, serikali ya Tanzania imetekeleza mambo mengi, ni wajibu wetu kushirikiana kumaliza vifo vinavyotokana uzazi na mimba za utotoni ili kila kijana atimize ndoto zake,”amesema.
Pia amebainisha kuwa serikali imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na inalenga kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake afisa kutoka UNFPA, Samwel Msokwa, akisoma taarifa ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika hilo, amesema kadri watu wanavyoongezeka changamoto nazo zinaongezeka ambapo katika ripoti hiyo inaonesha tatizo la mimba za utotoni duniani bado ni kubwa sana.
Ambalo mara kwa mara linaathiri mipango mbalimbali ya vijana wengi wanahitaji kupata fursa, au kujiendeleza zaidi katika elimu, huku vifo vya akina mama wajawazito navyo vikiongezeka.
“Ripoti inaeleza kinaga ubaga kuwa kuna tatizo la ukatili wa kijinsia licha ya taasisi mbalimbali kufanyiwa kazi, tuelekeze nguvu kukabiliana na tatizo hili,”amesema.
Naye, Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez amesema vifo vinavyotokana na uzazi bado ni changamoto hasa kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15-19.