…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali ya Ujerumani imetoa Euro milioni 6.0 kwa ajili ya kusaidia
miradi ya maji nchini ikiwemo kuboresha usambazaji na miundombinu ya maji.
Makubaliano hayo yalisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo na Mkuu wa Programu ya Maji katika Shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ) Dr. Johannes Schoeneberger
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Profesa Mkumbo aliwataka watumishi wa wizara hiyo kutekeleza yale yaliyomo katika makabiliano hayo bila visingizio.
“Serikali hii ni Serikali ya matokeo sio mchakato. Kama kununua magari basi tununue magari sio stori ndefu unajua tulishatoa tangazo sijui limeenda wapi tunataka matokeo,”amesema Prof.Mkumbo
Kwa upande wake Dr. Johannes Schoeneberger alisema kuwa fedha hizo si fedha za Serikali ya Ujerumani bali ni fedha za walipakodi wa Ujerumani na hivyo zitumike kuwasaidia walengwa ambao ni Watanzania.
“Matumizi, matokeo, utendaji, uhakikishaji yazingatie kuwa ni
ushirikiano huu unalenga katika kumfikia mwananchi kupitia Wizara