**************
Na Mwandishi wetu Katavi
Wadau wa mazao ya kilimo mkoani katavi wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na wenye viwanda wamepitisha azimio la kutosafirisha zao la mpunga kutoka nje ya mkoa huo na badala yake waliongezee thamani kwa kukoboa na kuuza mchele
kwa wastani mkoa wa katavi unazalisha tani laki mbili za mpunga kwa mwaka hali itakayowezesha kuongeza zaidi ya shilingi bilioni 1.1 ya mapato ya mkoa huo
wadau hao wamepitisha azimio hilo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya mpanda lengo likiwa ni pamoja na kuwa ongezeko la viwanda, kumwinua mkulima na kulinda ajira kwa wanawake na vijana
wakichangia hoja ya kutouza zao hilo nje ya mkoa wadau hao wamesema hata hivyo wamechelewa kufikia maamuzi yao ambapo kwa hivi sasa mapato mengi yanapotea kwa kuuza mpunga nje.
wametilia mkazo kuwa kuliongezea thamani zao hilo kutaboresha biasharaa ya mchele kwani licha ya baadhi ya mikoa kutegemea chakula kutoka katavi hata nchi jirani za komgo na burundi ni wateja wakubwa.
Katibu Tawala wa mkoa wa katavi bwana Abdallah Malela amesema maamuzi hayo yatawezesha katavi kuwa na ongezeko la viwanda vilivyo bora zaidi
Aidha amewataka wafanyabiashara kuondoa hofu ya kukosa soko la mchele kutokana na ukweli kwamba mahitaji ya chakula kwa mikoa ya jirani ni makubwa
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi bwana Juma Homera amesema kwa kuthibiti mpunga kutotoka nje ya mkoa kutasaidia kutunza mazingira kwani pumba inayopatikana inaweza kutumika kuchomea matofali