Home Mchanganyiko NDIKILO AIAGIZA HALMASHAURI YA MKURANGA KUWA MAKINI KUINGIA MKATABA NA MAWALA WABABAISHAJI

NDIKILO AIAGIZA HALMASHAURI YA MKURANGA KUWA MAKINI KUINGIA MKATABA NA MAWALA WABABAISHAJI

0

*****************

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Mkuranga,kuwa makini na mawakala wakusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuepuka kukimbia na fedha hatimae kuingia kwenye migogoro na kusababisha kukimbilia mahakamani .
Aidha ,ameitaka halmashauri hiyo kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kuongeza ufanisi.
Ndikilo alitoa maelekezo hayo, katika baraza maalum la madiwani kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) 2017/2018 ,wilayani Mkuranga.
Mkuu huyo wa mkoa alitaka wajipange kupata mawakala waaminifu wasioweza kupata fursa ya kukimbia na fedha za umma.
Ndikilo aliiasa halmashauri hiyo pia ,kuendelea kuongeza mapato ya ndani na kuwa na wigo wa vyanzo vya mapato ili kuinua mapato hayo.
Pamoja na hayo, aliielekeza menejimenti wilayani hapo kuhakikisha wanatekeleza hoja 32 ambazo hazijafungwa  hadi ifikapo agost 30 mwaka huu,ili ziweze kufungwa.
“Nimeona katika ya hoja ambazo hazijafungwa ,kuna kesi kama nne zinazohusu migogoro baina yenu na mawakala, hata mkikimbilia mahakamani haisaidii kama fedha zimeshaliwa ,mnapoteza fedha na muda,: Hivyo tafuteni mawakala wazuri kuepukana na shida hizi.”
“Kumekuwepo na changamoto ya kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo”:Hivyo basi wakurugenzi na watendaji simamieni ili sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kwa lengo la kusaidia mkaguzi akipita kusiwepo na dosari”alifafanua Ndikilo.
Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde alisema, hoja ambazo hazijafungwa nyingi zipo katika hatua ya utekelezaji hivyo wamepokea maagizo waliyopatiwa na aliahidi kuyafanyia kazi.
Awali kaimu katibu tawala wa mkoa huo, Shangwe Twamala alieleza, kutofungwa kwa hoja kunazalishwa na wakuu wa idara na wakuu wa vitengo ambao hawatekelezi majukumu yao kikamilifu kwa kutotunza na kuweka risiti za malipo.