WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Karukekere, Jimboni kwake
Mwibara, Wilayani Bunda, leo. Lugola aliwataka wanafunzi hao
kupenda masomo na kuacha utoro, na pia aliliagiza Jeshi la Polisi
wilayani huko, kuwakamata wazazi wanaowatumia wanafunzi
katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha
masomo yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akimuhoji Mratibu
Elimu Kata ya Namuhura, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda
(wapili kushoto), Ibrahimu Kadashali, kuhusu uwepo wa taarifa za
wanafunzi watoro, pamoja na wazazi kuwatumia wanafunzi katika
shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha
masomo yao. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Karukekere, Charles Manyama. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Karukekere, Jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, leo. Lugola aliliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo, kuwakamata wazazi wanaowatumia wanafunzi katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha masomo yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.