………………………Na.Alex Sonna,DodomaBENKI ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi gawio la Shilingi bilioni 1.2 kwa Serikali ya Tanzania pamoja na Wanahisa wengine wa benki hiyo.Gawio hilo limetokana na faida ambayo benki hiyo imeipata kutokana na shughuli zake katika kipindi cha mwaka 2017/2018.Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi gawio hilo iliyofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa alisema benki ya TPB imefanya vizuri mwaka jana kwa kupata faida ya Shilingi bilioni 17, na hivyo kuweza kutoa gawio la shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Mbili (1.2 bilioni) kwa Serikali pamoja na Wanahisa wake.“Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB najisikia faraja kusimamia benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 54 yaliyopo sokoni hivi sasa.Dkt.Mndolwa amesema kuwa Wanahisa wanaridhishwa na utendaji wa benki kwa kipindi hicho kwani benki ilifanikiwa kupata faida ya kiasi cha shilingi bilioni 17.2 kabla ya kodi.”Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wateja wetu ambao wameendelea kutuamini kwa kutumia huduma zetu kwa wingi.”Ahadi yetu kwao ni kwamba tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji yao”, alisema Dkt. MndolwaAkipokea gawio hilo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango aliipongeza benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 50 yaliyopo nchini.“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Benki ya TPB kwa gawio hili la shilingi bilioni Moja mlilolitoa kwa Serikali.”Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki hii kufanya hivyo, na kwasababu hiyo basi, nitoe pongezi kubwa na za dhati kwa uongozi wa TPB kwa gawio hili. Kutoa kwenu gawio kwa wanahisa wenu kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenya benki yenu.Hii ni ishara pia kuwa taasisi zinazomilikiwa na Serikali zinaweza kujiendesha kwa ufanisi na kwa faida, kiasi cha kuweza kutoa ushindani kwa taasisi nyingine za binafsi”, amesema Waziri MpangoWaziri Mpango pia alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa taasisi za Serikali kutumia huduma za kibenki kutoka benki hiyo kupitia matawi yake yaliyoenea nchi nzima ili kuiunga mkono.“Napenda kutoa wito kwa taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za Kibenki kote nchini Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB zilizoko mikoa yote nchini Tanzania.Benki ya TPB yenye matawi 75 nchi nzima inao wanahisa sita ambao ni Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shirika la Posta, Saccos ya Posta na Simu, Workers Compensation Fund pamoja na PSSSF. Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango, akipokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa.
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,akizungumza na wafanyakazi na wanahisa wakati wa kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa,akizungumza mara baada ya kukabidhi gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018
Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP,Sabasaba Moshing,akiongea na wafanyakazi na wanahisa wakati wa kutoa gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango, akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP,Sabasaba Moshing wa kwanza kulia na wa (katikati) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na wanahisa mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya TPB mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
BENKI ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi gawio la Shilingi bilioni 1.2 kwa Serikali ya Tanzania pamoja na Wanahisa wengine wa benki hiyo.
Gawio hilo limetokana na faida ambayo benki hiyo imeipata kutokana na shughuli zake katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi gawio hilo iliyofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa alisema benki ya TPB imefanya vizuri mwaka jana kwa kupata faida ya Shilingi bilioni 17, na hivyo kuweza kutoa gawio la shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Mbili (1.2 bilioni) kwa Serikali pamoja na Wanahisa wake.
“Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB najisikia faraja kusimamia benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 54 yaliyopo sokoni hivi sasa.
Dkt.Mndolwa amesema kuwa Wanahisa wanaridhishwa na utendaji wa benki kwa kipindi hicho kwani benki ilifanikiwa kupata faida ya kiasi cha shilingi bilioni 17.2 kabla ya kodi.
”Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wateja wetu ambao wameendelea kutuamini kwa kutumia huduma zetu kwa wingi.
”Ahadi yetu kwao ni kwamba tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji yao”, alisema Dkt. Mndolwa
Akipokea gawio hilo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango aliipongeza benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 50 yaliyopo nchini.
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Benki ya TPB kwa gawio hili la shilingi bilioni Moja mlilolitoa kwa Serikali.
”Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki hii kufanya hivyo, na kwasababu hiyo basi, nitoe pongezi kubwa na za dhati kwa uongozi wa TPB kwa gawio hili. Kutoa kwenu gawio kwa wanahisa wenu kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenya benki yenu.
Hii ni ishara pia kuwa taasisi zinazomilikiwa na Serikali zinaweza kujiendesha kwa ufanisi na kwa faida, kiasi cha kuweza kutoa ushindani kwa taasisi nyingine za binafsi”, amesema Waziri Mpango
Waziri Mpango pia alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa taasisi za Serikali kutumia huduma za kibenki kutoka benki hiyo kupitia matawi yake yaliyoenea nchi nzima ili kuiunga mkono.
“Napenda kutoa wito kwa taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za Kibenki kote nchini Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB zilizoko mikoa yote nchini Tanzania.
Benki ya TPB yenye matawi 75 nchi nzima inao wanahisa sita ambao ni Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shirika la Posta, Saccos ya Posta na Simu, Workers Compensation Fund pamoja na PSSSF.