Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya bidhaa iliyobuniwa na mmoja wa wanafunzi kutoka Chuo KIkuu cha Dar es Salaam, baada ya kutembelea banda hilo katika Maonesho ya biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kiwa Jijini Dar es Salaam.
**********
NA EMMANUEL MBATILO
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mh.. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wanataaluma kuendelea kukuza vipaji na Ubunifu unaofanywa na Wanafunzi ili kuweza kuleta Maendeleo katika Jamii.
Ameyasema hayo alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tarehe 6 Julai, 2019 katika Maonesho yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho ya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam
Mh.Kikwete aliweza kutembelea na kujionea kazi na Tafiti mbalimbali zilifanywa na Wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na kutoa sifa zake hasa kutokana na utaalamu walionao.