Wakazi wa vijiji vya Hanjawanu , Igando na Korinto kata ya Luduga wilani Wanging’ombe mkoani njombe wameiomba serikali kuwapelekea umeme katika vijiji vyao kwa madai ya kwamba ukuaji wa uchumi umekuwa hafifu kwasababu wanashindwa kuendana na mahitaji ya sasa ya sayansi na teknolojia
Vijiji hivyo ambavyo havija wahi kuwa na nishati ya umeme tangu uhuru vimetajwa kuporomoka zaidi kiuchumi na maendeleo kwa ujumla hatua ambayo inawasukuma wakazi wa kata ya Luduga yennye vijiji saba vyenye changamoto ya ukame kwa baadhi ya maeneo kuomba serikali kusogeza huduma hiyo kupitia mpango wa REA ili kutengeneza fursa za kuinua uchumi wao ambao unaporomoka kila uchwao.
Naomi Ngailo na Michael Aron ni baadhi ya wakazi na hapa wanatoa hisia zao kuhusu changamoto ya nishati ya umeme ambayo wamekuwa wakiishia kuitazama katika maeneo mengine ya wilaya ya Wanging’ombe .
Hassan Ngella ambaye ni diwani kata ya Luduga Anakiri kuwepo kwa changamoto hiyo anaiomba serikali kutatua changamoto hiyo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma ya mashine ya kusaga, salooni na kuendesha mitambo mingine ya uzalishaji.
Akiotolea Ufafanuzi wa changamoto hiyo kwa wananchi Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Mhandisi Gerson Lwenge amewatoa hofu wananchi kwa kudai kwamba serikali imeingiza vijiji hivyo katika mpango wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya tatu.