Na Asha Said, DAR ES SALAAM
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Agosti 23, mwaka huu wakati watani wa jadi, Simba na Yanga watamenyana Januari 4, mwakani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amesema hayo leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba.
Wambura amesema kwamba Ligi Kuu itafunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya mabingwa watetezi, Simba SC dhidi ya Azam FC washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Agosti 17, mwaka huu.
Alisema Ligi itafunguliwa rasmi Agosti 23, Simba ikianza kutetea taji na kuwania ubingwa wa tatu mfululizo kwa kucheza na JKT Tanzania, huku watani wao, Yanga wakifungua dimba na Ruvu Shooting ya Pwani.

Alisema upangaji wa ratiba ya Ligi hiyo umezingatia michuano mbalimbali ya kimataifa kwa upande wa timu za taifa na klabu za Simba, Yanga, Azam na KMC.
“Ratiba imepangwa kwa kuangalia mechi zote za Kimataifa, hakutakuwa na upanguaji wa mechi. Ikiwa ni pamoja na kila timu ijue haitakubaliwa kubadilishwa mechi zote zitachezwa kama zilizopangwa,” amesema Wambura.
Aidha, Wambura alisema kupunguzwa gharama kwa klabu zitakuwa zikicheza mechi zake kwa timu za mkoa mmoja kwa mfulululizo na si kwenda na kurudi.