Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akizungumza na wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon (hawapo
pichani) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni mratibu wa mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi na Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
(aliyeshika filimbi nyekundu) akionyesha ishara ya kuanza kwa mbio za Capital City Marathon kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.
Baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon wakijiandaa
kuanza mbio zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bw.Rashid Ally baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Baiskeli Km.22 za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bw.Godlisten Mmmary baada ya kuibuka mshindi wa kwanza
katika mbio za walemavu za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019
Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bi.Fabiola John baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio
za Km. 10 kwa wanawake za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019
Jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye
ulemavu Mhe.Antony Mavunde.
Mratibu wa Mbio za Capital City Marathon Bw.Nsolo Mlozi akitoa neon la
shukrani kwa washiriki wa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini
Dodoma.Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison
Mwakyembe.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison
Mwakyembe(Katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa mbio za Capital City Marathon kwa upande wa walemavu pamoja na viongozi wa Mkoa,Chama na Serikali baada ya kumalizika kwa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.
*************
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa watanzania kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupenda michezo kuanzia kushiriki,kushangilia pamoja na uhamasishaji ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio na maendeleo ya michezo hapa nchini na uwakilishi mzuri nje ya nchi.
Dkt.Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa anamuwakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan katika mashindano ya riadha ya Capital City Marathon ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi yetu imeanza kurudi katika ramani ya michezo kutokana na watanzania kushriki kwa wingi katika michezo mbalimbali.
“Nawapongeza sana Watanzania wamekuwa na ari kubwa sana ya kushirikiki michezo hasa riadha ambayo imetutangaza vyema nje ya nchi,ni matuamini yangu mtaendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia na michezo mingine vijana endeleeni kuchezakwa bidii zaidi kwakua michezo sasa ni chanzo kikubwa cha kipato”amesema Dkt.Mwakyembe.
Aidha Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa Taifa limekuwa na uwakilishi mzuri katika mchezo wa Soka kwani limepata nafasi ya kushiriki AFCON 2019,kuongezeka kwa timu zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika ambayo ni Simba na Yanga pamoja na Klabu Mbili zitakazoshiriki Kombe la Shirikisho ambazo ni Azam FC na KMC.
Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe ameiagiza Idara ya Maendeleo ya
Michezo kushirikiana na wadau kuwa na utaratibu wa kuandaa orodha ya wadhamini wanaojitokeza na namna wanavyodhamini mashindano mbalimbali ili kuweka kumbukumbuku vizuri na kutoa ushauri panapowezekana katika kuimarisha Sekta hiyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi mbali na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyotoa pamoja na washiriki waliojitokeza ameishauri jamii kuwa na
utaratibu wa kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ili
kujenga miili yao kwa kuimarisha afya lakini pia kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza ambayo kwa sasa yamekuwa yakiwatesa wananchi wengi.
Vilevile Bw.Nsolo ameongeza kuwa Capital City Marathon ilianza na kuwa na idadi
ndogo ya washiriki lakini mwaka huu idadi imeongezeka na kufikia washiriki 2,200
ambao kulingana na miundombinu imara ya Jiji la Dodoma wameweza kukimbia bila kupata changamoto yoyote.
Naye mshindi wa km 21 kwa upande wa wanaume Bw.Emmanuel Giniki amesema
kuwa mchezo wa riadha ni mchezo ambao unahitaji kuwa na mazoezi ya mara kwa mara ili kuweza kufanya vizuri ambapo amewashauri vijana wengi kujitokeza katika mashindano mbalimbali ya riadha yanayotokea ili kupata kipato pamoja na kupata ajira.
Mbio za Capital City Marathon zinafanyika kwa mara ya pili Jijini Dodoma ambapo
mwaka huu zimehusisha mbio za KM 22 Baiskeli,km.21wanawake na wanaume,km 10 wanawake na wanaume pamoja na km 5.