Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Rugby (hawapo pichani) wakati wa mahafali ya ukwata.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati msaada kwa mmoja ya wanafunzi wa chuo cha Rungemba walipofanya mahafari ya kidini.
( Picha na Denis Mlowe)
…………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati amechangia shilingi laki mbili (2) na kuahidi kununua kifaa cha muziki kwa wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya jamii, Lungemba, Mufindi zitakazotumika katika kurekodia albamu yao.
“Nitachangia shilingi laki 2 kwanza ili mmalize kurekodi nyimbo zenu za video. Na pia nitachangia kifaa cha muziki nitajaribu kutafuta cha aina gani kisha niwaletee”
Mhe. Kabati amechangia fedha hio wakati wa mahafali ya wanafunzi wa dhehebu la Ukwata, chuoni hapo.
Pamoja na mchango huo, Kabati amewataka wanafunzi wa chuoni hapo kujikita katika mambo ya kimaendeleo ikiwepo mafunzo ya ujasiriamali yatakayoweza kunyanyua kipato chao.
“Msiache kujiingiza katika mafunzo ya ujasiriamali mtakaposikia yanafanyika kwa sababu yatainua kipato chenu”
Awali akisoma risala kwa mgeni mwanafunzi anayehitimu, Grace Mhanga amebainisha changamoto zinazowakabili wanaukwata chuoni hapo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya muziki, laptop pamoja na pesa taslimu shilingi laki 2 kwa ajili ya kurekodia video.
“Sisi kama wanaukwata tunakosa pesa shilingi laki mbili pamoja na vifaa vya muziki vitakavyosaidia kuendeleza injili ya MUNGU”