NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka wananchi kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano chini Dakta John Pombe Magufuli imefanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake na Ilani yake ya uchaguzi wa Mwaka 2015 tofauti na propaganda za baadhi ya watu wanavyodai.
Mgumba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na katika vikao vya wajumbe wa CCM katika Maeneo ya Kinole.Tegetero na Kibungo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro.
Akizungumza na wajumbe hao kwa nyakati tofauti Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba ambae ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mashariki amesema kuwa serikali imefanya mambo mazuri katika kuwahudumia wananchi wake katika Jimbo hilo la Morogoro kusini Mashariki.
Amesema kuwa Baadhi ya miradi hiyo katika kipindi cha Miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano katika jimbo hilo ni pamoja kuunganisha mitandao ya Barabara,kutoa fedha kwaajili ya ujezni ya vituo vya afya,umaliziaji wa maboma na ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja mabweni ya wanafunzi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka wananachama wa chama cha Mapinduzi CCM kueleza mazuri yanayofanywa na serikali kwani wasipofanya hivyo baadhi ya watu wenye chuki na chama hicho wataeneza propaganda chafu kuwa CCM haijafanya lolote jambo ambalo halina ukweli.
Pia ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wanachama hao kuchagua viongozi wenye uchungu na CCM pamoja na wenye kujali maslahi ya wananchi watakao kuja kuwahudumia vizuri.
Kwa uapnde wao Baadhi ya madiwani na wana-CCM walimpongeza naibu waziri wa Kilimo katika kuwahudumia kwa kuwaletea maendeleo wananchi wake pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili.