***********
NA EMMANUEL MBATILO
Wananchi watakiwa kutumia vifaa ama bidhaa vinavyotengenezwa na Chuo cha ufundi Stadi VETA kwani vimekuwa vikitengeneza vifaa vilivyobora kwa matumizi bila kuathiri mazingira.
Ameyasema leo Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Bw.Peter Maduki baada ya kutembelea banda la VETA katika Maonesho ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kiwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari, Bw.Maduki amewataka Watanzania wawe na utamaduni wa kutumia elimu pamoja na vifaa vitokanavyo na VETA kwani kunaweza kuleta maendeleo hasa katika sekta ya Viwanda ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda.
“Nawaomba watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuendeleza fani walizonauza kwa kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi VETA kwani kutamuwezesha kuweza kupata ujuzi ambao utamsaidia kutengeneza bidhaa au kifaa kilichobora kwa maendeleo ya jamii”. Amesema Bw.Maduki.
Aidha Bw. Maduki ameongeza kuwa kwasasa walimu wa Ufundi Stadi ni wachache hivyo amewaomba watanzania waweze kujitokeza kwaajili yaq kusoma elimu ya ualimu wa ufundi Stadi ili kuweza kukuza na kueneza viwanda vya kutosha hapa nchini.