Home Biashara MAKAMU WA RAIS ALITEMBELEA BANDA LA BOT SABASABA

MAKAMU WA RAIS ALITEMBELEA BANDA LA BOT SABASABA

0

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki Kuu Sabasaba.

……………………………………………………

Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa wilayani Temeke.

Katika ziara hiyo ambayo ilifanyika mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo jana, Makamu wa Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi aliambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Innocent Bashungwa na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Mama Samia Suluhu Hassan alilakiwa na Naibu Gavana, Dkt. Bernard Kibesse ambaye alimpatia maelezo kuhusu kazi za Benki Kuu ya Tanzania na nafasi ya Benki Kuu katika kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa kauli mbiu ya maonesho; ‘Usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda’.

Katika maonesho ya mwaka huu, banda la Benki Kuu ni kubwa, pana, lenye mpangilio wa kuvutia na matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) inayowawezesha wananchi kujionea wenyewe kazi za Benki Kuu badala ya kutegemea tu maelezo kutoka kwa washiriki.

Zaidi ya wananchi 1500 wamekwishatembelea maonesho haya toka yalipoanza tarehe 28 Juni 2019. Aidha, menejimenti ya Benki Kuu imekuwa ikishirikiana na washiriki kutoka kurugenzi zao katika kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda la Benki Kuu.

Makamu wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Gavana, Dkt. Kibesse wakati alipokuwa katika meza ya Kurugenzi ya Utumishi na Uendeshaji. Kulia Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bw. Nassor Omar, akitoa maelezo kuhusu kazi za Kurugenzi hiyo huku Makamu wa Rais akifuatilia. Chini wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania wakiwa na Naibu Gavana, Dkt. Kibesse (aliyeshika kombe) katika picha ya pamoja mara baada ya Benki Kuu ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la Mamlaka za Usimamizi na Udhibiti katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.

Washiriki wa Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Bi. Laila Kisombe na Bw. Fidelis Mkatte wakiwahudumia wananchi na kulia ni muonekano wa banda la Benki Kuu.

Gavana wa Benki Kuu  ya Tanzania Profesa Florens Luoga akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa  benki hiyo kutoka dawati la malalamiko wakati waipotembelea maonesha ya biashara ya TANTRADE yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo.

Gavana wa Benki Kuu  ya Tanzania Profesa Florens Luoga akipata maelezo kutoka kwa Abdul Dollah Meneja Msaidizi wa Sarafu BOT wakati waipotembelea maonesha ya biashara ya TANTRADE yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo na kushoto ni Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina