Home Michezo Tabora Yaibuka kinara wa Mashindano ya UMITASHUMTA 2019

Tabora Yaibuka kinara wa Mashindano ya UMITASHUMTA 2019

0

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa zawadi ya kikombe kwa washindi wa mpira wa wavu wasichana timu ya mkoa wa Mtwara kwa mwakilishi wa mkoa huo jana

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana kwenye uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara

…………………….

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mkoa wa Tabora umefanikiwa kuwa mshindi wa jumla wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 baada ya timu zake kufanikiwa kufanya vizuri na hivyo kujipatia alama nyingi kuliko mikoa mingine 25 iliyoshiriki mashindano hayo mwaka huu.

Kwa mujibu wa matokeo ya washindi wa UMITASHUMTA mwaka 2019, mkoa wa Tabora ulifanya vizuri katika mchezo wa goli kwa wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, netiboli walishika nafasi ya pili, na kwaya walishika nafasi ya pili.

Kutokana na matokeo hayo mkoa wa Tabora ulifanikiwa kuwa wa kwanza baada ya kujizolea jumla ya alama 153, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam baada ya kujinyakulia alama 147.5.

 Mkoa wa Dar es salaam umekuwa ukifanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mfululizo, ambapo kwa mwaka huu, timu zake zilifanya vizuri katika michezo ya mpira wa goli wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, mpira wa mikono wavulana nafasi ya tatu, fani za ndani nafasi ya kwanza, wavu nafasi ya tatu na soka wameshika nafasi ya pili

Nafasi ya mshindi wa tatu imechukuliwa na mkoa wa Mara baada ya kupata alama 143.7 ambazo zimetokana na ushindi kwenuye michezo ya usafi na nidhamu wavulana kwa kushika nafasi ya kwanza, riadha wasichana nafasi ya pili, mpira wa mikono wavulana na wasichana nafasi ya kwanza na soka wasichana nafasi ya pili.

Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya nne ambapo timu zake zilifanya vizuri kwenye michezo ya riadha wasichana walishika nafasi ya kwanza, ngoma nafasi ya pili na soka kawaida nafasi ya tatu.

Nafasi ya tano ilichukuliwa na mkoa wa Geita ambapo timu yao ya soka iliifunga Dar es salaam kwa njia ya penati, huku nafasi ya sita ilikwenda Mbeya, Morogoro ilichukua nafasi ya saba, Manyara ilishika nafasi ya 8, Tanga ikashika nafasi ya 9 na Mtwara ilishika nafasi ya kumi.

Mkoa wa Kilimanjaro ulishika nafasi ya 11, Dodoma 12, Shinyanga 13, Pwani 14, Kagera 15, Lindi 16, Arusha 17, Simiyu 18, Songwe 19, Kigoma 19 na 20 Kigoma.

Mikoa mingine ni Singida iliyoshika nafasi ya 21, Katavi 22, Ruvuma 23, Iringa 24, Rukwa 25 na Njombe 26

Kilele cha mashindano ya UMITASHUMTA kilihitimishwa jana katika uwanja wa Nangwanda sijaona kwa hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo