Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Tixon Nzunda amekitembelea kikosi kazi kinachoangalia maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini na kuwataka kuzingatia weledi, haki za binadamu na utawala bora ili kupata mfumo utakaotoa haki na kuzingatia utawala wa sheria.
Bw. Nzunda ametoa rai hiyo alipokutana na kuzungumza na wataalamu kutoka serikalini na katika mashirika yasiyo ya serikali wanaoendelea na kazi ya kuangalia namna ya kuboresho mfumo wa haki jinai nchini jijini Dodoma.
“niwapongeze kwa kuwa sehemu ya kazi hii, nyinyi ni sehemu ya mabadiliko, kwa kazi hii lazima mzingatie weledi, uwazi, ukweli na haki za binadamu, ili wananchi ambao mmewaacha huko uraiani waweze kupata haki zao pale wanapostahili,” alisema na kuongeza kuwa mfumo unaofanyiwa maboresho lazima ulinde haki za wananchi.
Amesema ni matumaini ya Serikali kuwa kupitia maboresho hayo utapatikana Mfumo ambao utalinda haki za binadamu na kuzingatia utawala wa sheria kwa kuwezesha haki kutendeka na kupatikana baina ya watendaji na wananchi.
Be. Nzunda pia amewataka wataalamu hao kuzingatia uadilifu kwa kufanya yaliyo sahihi huku wakiwafikiria wananchi.
Amesema maboresho hayo yakizingatia mambo hayo yataleta Mfumo utakaomaliza tatizo la rushwa, mgongano baina ya taasisi na kuleta uwazi, kutenda haki kwa wananchi hivyo kuwa na mfumo wa watu ambao unazingatia utawala wa sheria