Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Christopher Bazivamo akifugua semina ya waandishi wa habari iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii kwenye hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam kuhusu mradi wa (50 Milioni African Women Speak Networking) unaotekelezwa katika nchi za jumuiya za (EAC), (ECOWAS) na (COMMESA) , Kulia ni JUvenari Ndimurirwo Mkurugenzi wa Fedha (EAC)
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh. Christopher Bazivamo akifugua semina ya waandishi wa habari iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii kwenye hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam kuhusu mradi wa (50 Milioni African Women Speak Networking)katikati ni ni Mary Makoffu Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC) na wa pili kutoka kushoto ni Ofisa Maendeleo Mwandamizi wa Wizara hiyo kutoka Idara ya Jinsia Mapunda John.
………………………………………….
NA JOHN BUKUKU
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh. Christopher Bazivamo amesema nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinatakiwa kuungana katika kila jambo ambalo linatekelezwa kwa manufaa ya watu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kuwa na nguvu ya pamoja katika mambo yetu.
Amesema ni vigumu sana kufanikiwa kama kila nchi itafanya jambo peke yake hasa utekelezaji wa miradi inayobuniwa na jumuiya kwa sababu umoja ni nguvu katika kila jambo linalohitaji mafanikio kama hili la kuinua kipato cha wanawake wajasiriamali kutoka Jumuiya zetu za (EAC) ECOWAS na COMMESA ambako mradi huu utatekelezwa.
Mh. Christopher Bazivamo ameyasema hayo wakati akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu mradi wa (50 Milioni African Women Speak Networking) unaotekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika nchi sita za jumuiya hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam mwanzoni mwa wiki hii .
Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na kazi moja ya kuwaunganisha wanawake wajasiriamali ili wapate taarifa muhimu za Biashara, Fedha na Masoko kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine barani Afrika zilizomo katika jumuiya za ECOWAS na COMMESA kwa kuwa taarifa hizo zitapatikana katika Tovuti (Website)hiyo .
Naye Ofisa Maendeleo Idara ya Jinsia na mratibu wa mradi huo hapa nchini Bw. Mapunda John Akifafanua zaidi kando ya semina hiyo amesema Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepewa jukumu la kuratibu mradi wa (50 Milioni African Women Speak Networking) hapa nchini ili kuwaunganisha wanawake wajasiriamali wapate taarifa muhimu za biashara na fedha kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine Barani Afrika.
Mapunda amesema mradi huo unatekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi zilizomo katika jumuiya za ECOWAS na COMMESA na lengo lake kubwa ni kuwawezesha wanawake kiuchumi na hususani wanawake wajasiriamali.
“Kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mradi huo unatekelezwa kwenye nchi zote sita. na katika nchi nyingine nje za nje ambazo ziko kwenye Jumuiya za (ECOWAS) na (COMMESA). Kuhusu kuwawezesha wanawake kiuchumi katika suala zima la kuwapatia taarifa muhimu ikiwa ni pamoja na taarifa za fedha na taarifa ambazo sio za fedha.
“Sasa kwa maana ya taarifa za fedha tunamaanisha taarifa kwa mfano za wapi mikopo inapatikana ,wapi grants zinapatikana lakini ili waweze kutumia kama mitaji kuendesha biashara zao lakini tunavyosema taarifa ambazo sio za fedha kuna taarifa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa wajasiriamali kuzipata,” amesema John.
Pia amesema taarifa zinazohusu masoko na mambo mengine ya kutambua thamani na wapi kwenye uhitaji na hata usalama wa biashara kwani kuna baadhi ya nchi nyakati za uchaguzi hahuko salama ,hivyo lazima wajasiriamali hao wawe na taarifa.
Amesisitiza kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuhakikisha ni namna gani taarifa hizo zitawafikia wanawake wajasiriamali na ndio maana matarajio ni kuandaliwa kwa Website ambayo ndani yake kutakuwa kunawekwa taarifa zote muhimu.
“Na kwamba si tu bali wanafikiria kwa kuwa na eneo moja la wajasiriamali kukutana watakuwa na mijadala mbalimbali kati ya wafanyabiashara wakubwa na wakati ikiwa pamoja na kubadilishana uzoefu,” amesema John.
Amefafanua kuwa wameona kuwa wanaweza kutengeneza Website nzuri na kuwekwa taarifa zote lakini kama wanawake wajasiriamali hawajui haitakuwa na maana yoyote.
Hivyo amesemani fursa muhimu kwao kukutana na vyombo vya habari kwani kwa kutumia njia zao za kufikisha taarifa watawafikishia wanawake wajasiriamali taarifa za nchiradi huo na wanafanya hivyo kwa kuamini kuna takribani ya wanawake milioni 500 na malengo ni kuwafikia wanawake asilimia 10 ambayo ukiiigiwa unapata wajasiriamali milioni 50 kwa jumuiya tatu ambazo kuna nchi 38.
“Wanawake wapo wengi,wapo ambao wamefanikiwa na wapo ambao hawajafanikiwa.Kwa kutumia Poto hii au Website tunaamini itakuww chachu ya maendeleo yao na nchi husika kwa ujumla,” amesema John.
Naibu Ktibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Christopher Bazivamo akifugua semina ya waandishi wa habari iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii kwenye hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam kuhusu mradi wa 50 Milioni African Women Spea, Kulia ni Kulia ni JUvenari Ndimurirwo Mkurugenzi wa Fedha (EAC) kushoto ni Mary Makoffu Mkurugenzi wa Idara ya Jamii (EAC)
Bw. Wilson Muyenzi Mratibu wa Mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari katika semina hiyo.
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada.
Washiriki wa semina hiyo wakijadiliana maazimio ya semina hiyo katika makundi.
Wilson Muyenzi Mratibu wa mradi wa 50 Milioni African Women Speak Networking kulia akiwa mmoja wa maofisa wa (EAC) katika semina hiyo.