Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (Wakwanza kushoto), Waziri Mkuu Mtaafu Mh. Mizengo Peter Pinda Wakipokea maelekezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Mobisol Bw.Farid Abdallah.
Mtambo wa Mobisol Solar ukiwa ndani ya banda la maonyesho la Kampuni ya Mobisol katika maonyesho ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa kampuni ya Mobisol Bi.Zaituni Mrisho akiwaelekeza wateja namna ikifanya kazi mtambo wa Mobisol Solar unavyoifanya kazi na kuleta faida kwa mtumiaji
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Mobisol akiwangoja wateja wanaofika katika banda hilo kwaajili ya kuona na kufahamu namna mtambo wa Mobisol Solar unavyofanya kazi
************
NA EMMANUEL MBATILO
Kampuni ya Mobisol ambayo inajihusisha na huuzaji wa Solar kwa matumizi nyumbani imeendelea kuwanufaisha wananchi baada ya kuwafikia watu 500,000 wanaofurahia mtambo wa solar kwa matumizi ya nyumbani tangu kampuni hiyo ilivyoanza shughuli zake Tanzania.
Mobisol imemfanya mjasilaimali kuendelea kufanya biashara zake kwa utaalamu wa hali ya juu hasa katika utumiaji wa Solar za kampuni hiyo.
Ameyasema hayo leo Mkandarasi wa Mauzo Mobisol, Bw.Wilson Moses katika Maonesho ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe blog, Bw.Moses amesema kuwa Mobisol imesaidia familia nyingi kuondokana na changamoto za kutokuwa na nishati ya umeme kwa muda mrefu. Kaya nyingi zimeweza kulipia mitambo yao kidogo kidogo kwa kutumia huduma za simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa.
“Wateja wengi wa Mobisol wanamiliki mitambo yao kwa sasa na wanapata umeme kwa ajili ya watoto wao kusoma usiku. Wengine wameanza kuonyesha filamu kwa kulipisha, wengine wananyoa yaani vinyozi ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea kipato kupitia mtambo wa Mobisol”. Amesema Bw.Moses.
Amesema kuwa umeme kutoka Mobisol ni mfumo wa umeme jua unaoendana na uchumi wa Mtanzania tofauti na umeme wa kawaida ambao unaweza kuwa gharam, huchukua muda kupata na unaweza kukatika mara kwa mara.Umeme jua ni bei nafuu,rahisi kupata na rafiki wa mazingira.
“Mobisol inatoa mitambo ya sola yenye ubora wa hali ya juu katika aina nne za ukubwa tofauti ambayo inaanzia wati 40 mpaka 200. Kifurushi cha Mobisol kinajumuisha panel ya sola,betri,kontrola ya sola,taa,redio,tochi,luninga ya DC na waya za kuchajia simu”. Ameongeza Bw.Moses.
Pamoja na hayo Bw.Moses amesema kuwa takribani robo ya wateja wao wamechagua kutumia mitambo ya Mobisol kwa kutengeneza kipato cha ziada kwa kuendesha biashara ndogondogo