Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida la afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jarida la afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo,upande wa kulia ni Mhariri Mkuu Msaidizi Jarida la Afya ya Jamii Tanzania Dr.Julius Massaga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akifungua jarida mara baada ya kulizindua ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo,upande wa kulia ni Mhariri Mkuu Msaidizi Jarida la Afya ya Jamii Tanzania Dr.Julius Massaga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akiwa na baadhi ya viongozi wakionyesha Jarida la Afya ya jamii mara baada ya kulizindua ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Mhariri Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa Jarida hilo Prof.Muhammad Kambi akimueleza jambo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,mara baada ya kuzindua Jarida la Afya ya jamii mara ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akimsikiliza Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa Jarida hilo Prof.Muhammad Kambi mara baada ya kuzindua Jarida la Afya ya jamii mara ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Sehemu ya Muonekano wa Jarida la Afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Sehemu ya wadau wakifatilia uzinduzi wa Jarida la Afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, imezindua jarida la afya ya jamii, ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa kisayansi na kuziweka katika lugha nyepesi ambayo itaeleweka na kila mtu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida hilo, Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema jarida hilo litakuwa na umuhimu mkubwa sana hasa katika kuleta taarifa kwa jamii zinazotoka katika wizara hilo.
Amewaelekeza wataalamu, wahariri wa vyombo vya habari na wakurugenzi kutoa taarifa za afya katika jarida hilo ili taarifa zao ziweze kuwafikia wananchi kwa urahisi kupitia jarida hilo zitakazo wasaidia wananchi.
“Kuanzishwa kwa jarida hili kutasaidia sana kwa wananchi kupata taarifa sahihi zilizotoka katika wizara hiyo na kuzijua kwa undani, pia ni wakati sasa kwa wataalamu, wakurugenzi na wahariri wa vyombo vya habari kutoa taarifa kupitia jarida hili” amesema Ummy.
Pia amewaagiza wataalamu wa jarida hilo kuhakikisha jarida hilo linapatikana kielecronic ili kila mtu aweze kulipata jarida hilo.
“Ni toe wito kwa wasimamizi wa jarida hili mhakikishe jarida hili linapatikana kielectrinic mimi pia sio muumini wa kusoma majarida ila kama likipatikana kielectronic na mimi nitaweza kupata taarifa hizo” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa yakuambukizwa na yasiyoya kuambukizwa Dkt Janneth Mghamba , jarida hilo ambalo linatumia takwimu mbalimbali hapa nchini ambazo zinachambuliwa kisayansi na kuziweka katika lugha nyepesi.
“Jarida hili litatumia kutoa taarifa ambazo zimethibitishwa na ambazo zimechambuliwa kisayansi ambazo zitakuwa zimewekwa katika mfumo rahisi na mwepesi” amesema Mghamba
Amesema jarida hilo litasaidia kujua nini wizara inafanya na namna wao wanavyoweza kushiriki katika kudhibiti magonjwa hayo na namna ya kuepukana magonjwa hatarishi.
Amesema jarida hilo ni la kwanza na litakuwa kama kioo cha wizara ya afya, kioo cha sera kioo cha kutoa mwelekeo,ufasaha wa sayansi mbalimbali ambazo zinafanyika ndani na nje ya nchi.
Nae Mhariri msaidizi wa jarida hilo Dkt Julius Massaga, amesema jarida hilo limetengenezwa kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kuzinduliwa hivi leo litasaidia kutoa taarifa sahihi kwa jamii ambazo zimethibitishwa na wizara ya afya.
Jarida hilo ambalo limefadhiliwa na CDC Foundation kutoka Marekani na litakuwa linatoka mara nne kwa mwaka, lengo ni kutoa taarifa sahihi zinazoandaliwa na wizara ya afya kuwafikia wananchi kwa urahisi.
Amewataka wadau kuchangamkia fulsa hiyo kwa ajiri ya kutoa taarifa zao ili ziweze kuwafikia wananchi kiurahisi na kuzijua taarifa hizo ambazo zitakuwa zimethibitishwa na wizara na zitakuwa za uhakika.
“Ni wakati wa wadau sasa kujitokeza kuchangamkia fulsa hii kwa kuleta taarifa ili taarifa zao ziwafikie wadau wao kwa sababu zitakuwa zinatoka katika sehemu sahihi” amesema Massaga