NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WATU wawili wamefariki dunia mkoani Pwani ,kutokana na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka.
Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo.
Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema Kimiti aliuawa huko Malivundo ,Talawanda ,Chalinze, ambapo mtiliwa shaka Said Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa .
Alisema ,baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya tecno ,solar panel moja,shuka na baiskeli.
“Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka moja”alifafanua Wankyo.
Katika tukio jingine ,Wankyo alieleza Ngurai Waziri (33) mfugaji huko Msolwa kijiji cha Lukenge aliuawa kwa kukatwa na visu.
Kamanda huyo alibainisha, mtiliwa shaka David Mwanje (28) , Thomas Gau (25) na Magoma Ramadhani Mbwiga (32) wamekamatwa na katika mahojiano ya awali watuhumiwa hao wamedai marehemu alikuwa mwizi wa mifugo na alikuwa kero katika wizi wa mifugo.