Mwalimu wa Madereva wa Magari Makubwa Bw.William Munuo akionyesha ni namna gani teknolojia ya taa za barabarani zinaweza kufanya kazi kuokoa ajali ambazo zinaweza kutokea kwa askari wa barabarani.
Mfano wa mradi wa barabarani za juu pamoja na taa za barabarani ambazo zinaweza kusaidia kuondokana na ajali mbalimbali.
***********
NA EMMANUEL MBATILO
Chuo cha Ufundi VETA Kilichopo Kihonda mkoani Morogoro kupitia vijana wao wamebuni teknolojia ya taa za kuongoza magari barabarani zinazoongozwa na binadamu ili kuweza kupunguza ajali ambazo wanazipata askari wa usalama barabarani.
Ameyasema hayo leo Mwalimu wa Madereva wa Magari Makubwa Bw.William Munuo katika maonyesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe Blog, Bw.Munuo amesema kuwa ili kuweza kupunguza ajali za barabarani wameamua kuleta teknolojia hiyo ili kumrahisishia askari wa usalama barabarani kuelekeza masafara wa magari kwa kutumia swichi ambayo itakuwepo katika nguzo ya taa za barabarani ambayo itazima na kuruhusu magari kupita.
“Tumeona mara kwa mara askari wa usalama barabarani wanakumbwa na gadhia ya kugongwa na magari kutokana na uzembe wa madereva, gari kupata itirafu au dereva kuwa amechoka basi unakuta askari wetu wanapata ajari na kuweza kufa au kupata ulemavu”. Amesema Bw. Munuo.
Aidha Bw. Munuo amesema kuwa teknolojia hiyo itamfanya askari kubonyeza swichi na kuruhusu magari au kusimamisha magari katika sehemu iliyozidiwa.
Bw.Munuo ameongeza kuwa nchi yetu inaingia kwenye uchumi wa kati kitengo cha usafirishaji ni sehemu muhimu katika kufikia uchumi huo hivyo wale ambao wanafanya kazi ya kusafirisha mazao kutoka shambani kupeleka viwandani wapewe elimu ya usalama barabarani.