Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.
MAMLAKA ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, mkoa wa Dodoma, imemuamuru mkandarasi wa kampuni ya JUIN COMPANY LIMITED, inayotekeleza mradi wa maji katika kijiji cha kelema kuu wilayani Chemba, mkoani Dodoma kurejesha malipo zidifu iliyolipwa kampuni hiyo, na kutekeleza mradi huo kwa kiwango cha chini.
Akitoa taarifa kwa wanahabari ya robo ya 4 ya mwaka, kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mkandarasi huyo alilipwa fedha zidifu katika kutekeleza mradi huo wa maji na kuutekeleza chini ya kiwango.
“Katika uchunguzi wetu tulibaini thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kuto toa maji” amesema.
Amebainisha kuwa mkandarasi wa mradi huo ameridhia na amekubali kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo july mosi anaanza kazi ya kubadili mmabomba na kuweka yanayohitajika, na kurejesha malipo zidifu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni sitini na saba(67), na mradi huo unathamani ya shilingi 222,978,680, na ulitakiwa kukamilika tangu mwaka 2015.
Pia TAKUKURU imemtia nguvuni Mkurugenzi wa GLOBAL SPACE EAST AFRICA LIMITED, Bwana Gaston Meltus Francis aliyekuwa akitafutwa kwa kampuni yake kulipwa isivyohalali kiasi cha 86,405,205 aliyekuwa anajenga kituo cha afya cha Mima Wilayani Mpwapwa, na kazi hiyo haikufanyika.
Pia imefanikiwa kuzirejesha serikalini jumla ya shilingi milioni 11,877,353 zilizolipwa kinyume na utaratibu zilizokuwa zikiingia katika akaunti ya mwalimu ambaye tayari ameshafariki.
Pia amesema mkazo mmkubwa umewekwa katika kuwaanda wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa bila kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi huo wananchi yameaswa kuchagua viongozi waadilifu na wanaochukia rushwa.
Katika robo hii ya mwaka imekagua na kufuatilia miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi 32,545,418,116, ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo yalionekana kufanya vizuri.
“Katika robo ya tajwa TAKUKURU mkoa wa Dodoma imefuatilia na kukagua miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi 32,545,418,116, ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo yalionekana kufanya vizuri” amesema.
Amebainisha kuwa kwa kipindi hiki TAKUKURU ilipokea taarifa mia moja za rushwa mia moja therathini na tano(135) na makosa mengineyo ambapo, ambapo katika sekta ya ardhi ndio iliongoza kwa asilimia 36, zikifuatiwa zikifuatiwa na serikali za mitaa kwa asilimia 31.
Aidha amewataka wananchi kuwa waangalifu na vitendo vya rushwa hasa kwa wale ambao wanajifanya kuwa ni maafisa wa TAKUKURU na kupiga simu na kuwa tisha badala yake watoe taarifa katika mamlaka hiyo.
Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.MAMLAKA ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, mkoa wa Dodoma, imemuamuru mkandarasi wa kampuni ya JUIN COMPANY LIMITED, inayotekeleza mradi wa maji katika kijiji cha kelema kuu wilayani Chemba, mkoani Dodoma kurejesha malipo zidifu iliyolipwa kampuni hiyo, na kutekeleza mradi huo kwa kiwango cha chini.Akitoa taarifa kwa wanahabari ya robo ya 4 ya mwaka, kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mkandarasi huyo alilipwa fedha zidifu katika kutekeleza mradi huo wa maji na kuutekeleza chini ya kiwango.“Katika uchunguzi wetu tulibaini thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kuto toa maji” amesema.Amebainisha kuwa mkandarasi wa mradi huo ameridhia na amekubali kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo july mosi anaanza kazi ya kubadili mmabomba na kuweka yanayohitajika, na kurejesha malipo zidifu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni sitini na saba(67), na mradi huo unathamani ya shilingi 222,978,680, na ulitakiwa kukamilika tangu mwaka 2015.Pia TAKUKURU imemtia nguvuni Mkurugenzi wa GLOBAL SPACE EAST AFRICA LIMITED, Bwana Gaston Meltus Francis aliyekuwa akitafutwa kwa kampuni yake kulipwa isivyohalali kiasi cha 86,405,205 aliyekuwa anajenga kituo cha afya cha Mima Wilayani Mpwapwa, na kazi hiyo haikufanyika.Pia imefanikiwa kuzirejesha serikalini jumla ya shilingi milioni 11,877,353 zilizolipwa kinyume na utaratibu zilizokuwa zikiingia katika akaunti ya mwalimu ambaye tayari ameshafariki.Pia amesema mkazo mmkubwa umewekwa katika kuwaanda wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa bila kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi huo wananchi yameaswa kuchagua viongozi waadilifu na wanaochukia rushwa.Katika robo hii ya mwaka imekagua na kufuatilia miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi 32,545,418,116, ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo yalionekana kufanya vizuri.“Katika robo ya tajwa TAKUKURU mkoa wa Dodoma imefuatilia na kukagua miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi 32,545,418,116, ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo yalionekana kufanya vizuri” amesema.Amebainisha kuwa kwa kipindi hiki TAKUKURU ilipokea taarifa mia moja za rushwa mia moja therathini na tano(135) na makosa mengineyo ambapo, ambapo katika sekta ya ardhi ndio iliongoza kwa asilimia 36, zikifuatiwa zikifuatiwa na serikali za mitaa kwa asilimia 31.Aidha amewataka wananchi kuwa waangalifu na vitendo vya rushwa hasa kwa wale ambao wanajifanya kuwa ni maafisa wa TAKUKURU na kupiga simu na kuwa tisha badala yake watoe taarifa katika mamlaka hiyo.