Bw. Adam Duma akiwa na wanafunzi wa shule za sekondari baada ya kufika kufahamu ni namna gani teknolojia ya SmartCalss inaweza kufanya kazi.
Bw. Adam Duma akiwa anasubiri wateja wake katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika maonyesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
*****************
NA EMMANUEL MBATILO
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameandaa teknolojia hiitwayo SmartClass ambayo itamuwezesha Mwananchi au Kampuni kuweza kupata elimu ya ujuzi wowote anaoutaka au kufundisha.
Ameyasema hayo leo Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw.Adam Duma katika Maonyesho ya biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe Blog, mwanafunzi huyo amesema kuwa teknolojia hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika sekta ya teknolojia kwenye masuala mbalimbali kama Afya, Viwanda pamoja na uhamasishaji.
“SmartClass imeona ni namna vipi inaweza kuwapa fursa watanzania kuweza kupata elimu kupitia internet hasa kwa wale ambao wamemaliza Chuo au kwa wale ambao wamekuwa na ujuzi binafsi hivyo kuweza kushirikiana na wengine ili kuleta maendeleo hasa ya viwanda kuliko kubaki navyo tu”. Amesema Bw.Duma.
Aidha Bw.Duma amesema kuwa kutokana na wakulima wengi kukwama katika kilimo na kuwafanya kukata tamaa hivyo uwepo wa teknolojia hiyo itaweza kusaidia wakulima kuweza kujifunza namna gani wanaweza kuendesha kilimo kwa kupata elimu iliyobora kupitia SmartClass.
Bw.Duma amewaomba wananchi hasa vijana waweze kutumia fursa hiyo na wasisubiri tu kuajiliwa kwani fursa hii itaweza kumsaidia hasa kwa yule ambaye amekuwa na ujuzi pasipoweza kuutumia kwaajili ya kuelimisha wengine.