NJOMBE
Serikali mkoani Njombe imesema imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya bil 1.2 kwa vikundi 561 vya wanawake ,vijana na walemavu katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo hutolewa kila mwaka na halmashauri kutokana kwenye asimilia 10 ya mapato ya ndani.
Akizungumza katika kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe mkuu wa mkoa huo Christopher Olesendeka amesema serikali imeendelea kurahisisha mazingira ya wajasiriamali na biashara kwa ujumla kwa kuendelea kuhamasiaha uwekezaji na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kukuza mitaji yao.
Mbali na mikopo Olesendeka pia amesema katika mwaka wa fedha ulioisha juni serikali imefanikiwa kutekeleza ilani ya chama katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara zote zinazounganisha wilaya , maji, elimu pamoja na utoaji wa fedha na miradi kwa kaya masikini kupitia mpango wa TASAF hatua ambayo imehimarisha huduma na maisha kwa wakazi wa Njombe.
Katika kikao hicho pia wametambulishwa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Fakih Lulandala na Nelson Kyando aliyekuwa katibu wa ACT akitokea CHEDEMA ambao wanapata fursa ya kueleza sababu ya kujiunga na chama cha mapinduzi huku zaidi wakikosoa mfumo wa uongozi ambao wamedai umetawaliwa na timu pamoja na ubinafsi.
Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala ameagiza viongozi na wanachama wote kujipanga ili kiweze kuibuka kidedea wakati huo huo mkuu wa mkoa anatumia fursa hiyo kutoa maendeleo ya zoezi la ukugawaji wa vitambulisho kutoka asilimia 20 hadi 60 sasa.