Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Doris Muhimbila akitoa maelezo kwa wananchi wakati kampeni ya Mnada kwa Mnada mkoani Kilimanjaro.
Afisa Kusajili wa NIDA Mkoani wa Kilimanjaro. Abubakar kalinga akitoa maelezo wakati wananchi waliofika katika kampeni ya TCRA ya Mnada kwa Mnada.
Afisa wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandao akitoa maelezo kwa mwananchi kuhusiana na makosa ya mtandaoni yanayotokana na matumizi mabaya ya simu.
Wananchi wakiwa katika Foleni kwa ajili ya vitambulisho vya NIDA.
**************
Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini Julius Felix amesema ni fursa kwa wananchi wa Kilimanjaro kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.
Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.
Felix mesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
“TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema ni fursa kwa wananchi wa Kilimanjaro kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.
Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.
Amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
“TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” Felix