Home Mchanganyiko WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZA LA MKOA WA NJOMBE WAPEWA MISAADA YA KIBINADAMU

WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZA LA MKOA WA NJOMBE WAPEWA MISAADA YA KIBINADAMU

0

IMG_20190628_125734_2.jpgIMG_20190628_125731_2.jpgIMG_20190628_125936_6.jpg

NJOMBE

Shirika lisilo la kiserikali la Njombe youth development organization NJOYODEO kwa kushirikiana na umoja wa chama vijana wa chama cha mapinduzi mkoani Njombe umewatembelea wafungwa na mahabusu katika gereza la mkoa huo na kutoa misaada ya kibinadamu ikiwemo vyakula ili kuwaondolea dhana ya kwamba kundi hilo limesahaulika katika jamii.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo mkuu wa gereza la mkoa wa Njombe SP Charles Mhinga amesema idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu gerezani hapo wanakabiliwa kesi za mauaji ambazo chanzo chake ni migogoro ya ardhi, ushirikina na tamaa ya utajiri na kwamba wadau na serikali zinapaswa kuongeza kasi ya utoaji wa elimu kwa jamii .

Mhinga amesema gereza linakabiliwa na changamoto nyingi hivyo msaada uliotolewa na wadau hao utasaidia kupunguza changamoto kwa kuwa kulikuwa na upungufu mkubwa wa mablanketi, mashuka, kandambili , dawa za meno na miswaki huku akiwataka wadau wengi zaidi kujitokeza kuwasaidia pindi wanapoguswa kufanya hivyo.

Mbali na changamoto za wafungwa na mahabusu mkuu huyo wa gereza pia amesema wanakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi askari magereza na kueleza jitihada zinazochukuliwa kuipunguza ambapo amesema tayari usafishaji wa eneo la ujenzi wa nyumba umeanza hivyo mchango wa hali na mali unatakiwa.

Kwa upande wake Hamis Kasapa ambaye ni mkurugenzi wa NJOYODEO na katibu wa umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Njombe Amos Kusakula wanataja sababu zilizowagusa kutembelea , kuzungumza nao na kutoa misaada hiyo ya kibinadamu katika gereza hilo ni uwepo wa idadi kubwa ya vijana waliofungwa pamoja na mahabusu jambo ambalo linaonyesha kundi la vijana ambalo ndiyo nguvu kazi ya taifa lipo hatarini kuishia gerezani .

Katika hatua nyingine suala la usajiri wa vitamburisho vya taifa limewekwa wazi kwamba limekuwa halifanyiki katika maeneo mengi ya magereza jambo ambalo linawapa wakati mgumu wafungwa wanapo achiwa huru pindi wawapo mtaani wakitakiwa kutumia vitamburisho hivyo jambo ambalo linachukuliwa na kuahidi kufikishwa kwa wahusika kama ambavyo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa  Njombe Nehemia Tweve anavyo eleza umuhimu wa vitamburisho hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa gereza hilo zaidi ya asilimia 90 ya wafungwa wake na mahabusu ni vijana na wana kabiliwa na kesi za za mauaji