*****************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya nchini Italia, Ac Milan imefungiwa kushiriki michuano ya ulaya msimu ujao.
Hiyo ni baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria ya Financial Fair Play rules, imethibitisha mahakama inayoshughulikia masuala ya kimichezo (Court of Arbitration for Sport).
Club hiyo imefikia makubaliano na mahakama iyo kuwa endapo wanataka kushiriki michuano hiyo ya ulaya msimu ujao, watatakiwa kujiimarisha kwenye maswala ya mapato na matumizi ama sivyo watafungiwa tena kwa Mara nyingine. Na hivyo wanatakiwa kuuza wachezaji ili waingize pato kwenye timu.
Wakati Milan wakikutwa na rungu hilo club ya Torino imekua furaha kwao kwani wameliziba pengo Lao na watashiriki Europa league msimu ujao wakianzia hatua ya mtoano kabla ya ile ya makundi.