Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM- Zanzibar,
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein , Katibu Mkuu wa CCM
Dkt. Bashiru Ally, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Phillip Mangula wakiimba
wimbo wa Chama mara baada ya kuwasili ukumbini katika kikao cha Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Ccm Taifa (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-
Zanzibar Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohhamed Shein wakati wa kikao
cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia jambo katika cha halimashauri kuu ya Chama hicho
(NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na Waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa
halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Taifa Mizengo Pinda mara baada ya kikao
cha NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019
Wajumbe wa halimashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wakiimba
wimbo wa Chama mara baada ya kuwasili ukumbini Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam.
******************
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana
CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi
leo Jijini Dar es Salaam chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
\
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni mkutano wa kawaida
kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kikao pamoja na mambo mengine
kimefanya uchaguzi wa kujaza nafasi moja iliyokuwa wazi ya Mjumbe
wa Kamati Kuu na kuteua wanachama wa CCM wanao omba dhamana
ya uongozi katika Chama, Jumuia na Serikali.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kwa kauli moja kimeazimia
kuwapongeza Wanachama wa CCM na Viongozi kwa kazi nzuri ya
kufuatilia utekelezaji wa ilani kote nchini Tanzania.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa
kauli moja kupongeza Serikali za CCM za Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph
Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na
Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani na
unaokwenda na wakati huku tukiwa tumepata mafanikio makubwa ya
kuimarisha kiwango cha ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.1 na 7.3
mtawalia ambao ni jumuishi.
Kwa kauli moja wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT)
wamewapongeza viongozi wawakilishi wa wananchi wanaotokana na
CCM kwa kuendelea kuwa daraja kati ya wananchi na Serikali ya CCM
ambayo wananchi wameichagua. Kikao cha HKT pia kimewapongeza
Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM kwa kusimama kidete
kujadili mipango na kupitisha bajeti za Serikali zenye mrengo wa
kuwainua wananchi kutoka hali duni kwenda hali bora zaidi ikiwa ni
sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.