Shirika la umeme Tanesco kanda ya kaskazini leo limewakutanisha wamiliki wa viwanda ,wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa mikoa ya kanda hiyo ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali ambazo wafanya biashara hao wanakumbana nazo katika utendaji wao wa kazi ili kuimarisha sekta ya nishati na ukuzaji wa viwanda nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha AICC mkoani hapa meneja wa shirika hilo kanda ya kaskazini Stella Hiza alisema kuwa mkutano huo utatengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuweza kupata kuwa na umeme wa uhakika kwa kila kanda.
Amesema shirika la umeme Tanesco kanda ya kaskazini limepeleka mradi wa umeme kwa baadhi ya maeneo jijini Arusha ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili 2.6 mpaka kukamilika kwakwe.
Kwa upande wao baadhi ya mameneja kutoka kanda ya kaskazini wamesema kuwa shirika la umeme Tanesco wanaimarisha miundo mbinu ili kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi na kuondoa na kutatua changamoto zinazowakabili wateja wao.
“sisi kama shirika la tanesco tunawategemea sana wateja wetu wakubwa katika kukusanya mapato ya shirika kwani zaidi ya asilimia 40% ya mapato yetu yanatoka kwa wawekezaji pamoja na wenye viwanda na mapato haya yanatusaidia kuendesha huduma zetu pamoja na kukuza mapato ya nchi” Hiza
Alisema kuwa kwa upande wa Arusha wawekezaji wenye viwanda wapo 335 ambao ni sawa na asilimia 41%,Kilimanjaro ikiwa na wateja wakubwa 101 ambao wanachangia kwa asilimia 71% huku mkoa wa Tanga 117 ambao wanachangia kwa asilimia 64%.
Naye meneja wa Tanesco mkoa wa Kagera Fransis Martin aliwasihi wananchi ambao wanaiba umeme pamoja na wale wapoteza waache mara moja kwani kwakufanya hivyo wanapoteza mapato ya nchi
“katika jitiada za kupunguza wizi wa umeme tanesco imebadilisha teknolojia ya umeme katika hatua mbalimbali ikiwemo kubadilisha teknolojia mita katika hatua mbalimbali yakwanza kuwabadilisha wateja wa kawaida kutumia luku ,kutumia mita ambazo zinaakili yaani mita ambazo zinajitetea ambapo mtu akiigusa zinauwezo wa kutuma sms kwa watendaji wa shirika ili watendaji wafatilie”alisema Martin
Kwa upande wake mmoja wa wawekezaji kutoka SBC Peter Kalembo Aliipongeza sana Tanesco na kusema kuwa huduma inayotolewa na shirika hilo inakithi matarajia kwani changamoto ya umeme kukatika kwa sasa imepungua ,na hii imetokana na kutambua wajibu wao kwani kwa kipindi hichi huduma zao zinarizisha.
Awali Alidai kuwa kulikuwa na shida kubwa kwa shirika hili kutoa huduma tarajio kwa wateja hivyo kufanya wawekezaji wengi kushindwa kuwekeza na wengine wakaona huduma ya umeme inawapa shida lakini kwa sasa wataweza kuwekeza maana tatizo hilo limeisha na katika eneo la uwekezaji sera zinabadilika za kushawishi wawekezaji waweze kuja kuwekeza na kufanya biashara kwa pamoja .
Akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema tangu kuanzishwa kwa nchi yetu shirika limeshazalisha mega wat 1500 na katika hilo hadi kufikia sasa megawat 1300ndio zinatumika tunauwiano wa zaidi wa megawat 200 ambazo azitumiki
Aidha aliwasihi Tanesco kutembelea maeneo ambayo yametegwa kwa ajili ya uwekezaji yaliopo katika cha Malula wilayani Arumeru ambapo kina ekari zaidi ya mia Tano nakuwekeza miundombinu ya umeme kwani eneo hilo lina fursa mbalimbali za uwekezaji kwani katika eneo hilo kunatarajiwa kujegwa bandari kavu ya Tanga.
Mkutano huo ambao umefunguliwa leo umeshirikisha mameneja wa Tanesco kanda ya kaskazini ,Wawekezaji,Wafanyabiashara wa Viwanda wakubwa ambao wametoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Manyara