mwenyekiti wa chama cha Tanzania labour Part jimbo la vunjo Wilbard Moshi akiongea katika msiba huo
mwenyekiti wa chama cha Tanzania labour Part jimbo la vunjo Wilbard Moshi akimkabidhi rambirambi kama mkono wa pole mtoto wa Marehemu Jemsi Mmanyi.
******************
Na Woinde Shizza ,Arusha
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party Taifa Agustino Mrema amempongeza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kasi ,na jinsi anavyofanya kazi za kusaidia jamii haswa watu wa hali ya chini.
Ameyabainisha hayo jana mkoani Kilimanjaro katika kata ya Kahe kijiji cha Horia ndani ya jimbo la Vunjo wakati akihutubia katika msiba wa wa aliekuwa msaidizi wa mwenyekiti wa cha Tanzania Labor Part (TLP)taifa ambapo pia kwa upande wa chama hicho alikuwa mwanaharakati maarufu Anael Meleckizedek Mmanyi aliefariki dunia May 21 katikia hospital ya Mawenzi ambapo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo
Alibainisha kuwa kasi ambayo Rais anaenda nayo inaridhisha kwa kiasi kikubwa na anaamini kabisa kwa kuwa ni mtetezi wa wanyonge ata wakumbuka pia wananchi wa Vunjo na kusaidia kutatua matatizo ambayo yanayowakabili wananchi hao hivyo aliwahimiza wananchi hao kuendelea kumuunga mkono na katika kumuunga mkono wanataki kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi November mwaka huu
Akiongelea msiba huo alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za msiba wa katibu mwenezi wa wa wilaya ya moshi kupitia chama cha TLP jimbo la Vunjo kwani alikuwa mchapa kazi mzuri na mtu asie yumbishwa yumbishwa na maneno wala kitu chochote na alikua mpenda maendeleo kujiusisha na ujenzi wa taifa kwa kutumia vyema nguvu zake kuakikisha kwamba wananchi wanapata maendeleo bia kujali chama kilichopo madarakani kuanzia kazi ya kijiji kata hadi jimbo na taifa kwa ujumla .
Alibainisha kuwa katibu mwenezi huyu alikuwa ni mtu ambaye anaamasisha wananchi kuendelea kulinda amani ilioasisiwa na baba wa taifa huku akisisitiza zaidi amani ndio kitu pekee ambacho wananchi wanaweza kujivunia kwani nchi yenye amani lazima iwe na
Kwa upande wake kiongozi wa kiroho kutoka kanisa la KKKT Usharika wa Kahe aliye ongoza ibada iyo Mwinjilisti Rabson Mlay amitaka jamii iyo ya kijiji cha Horia kuiga mema ya marehemu katika huai wake kwani alikua mchapa kazi na mwamasishahji mzuri wa mikutano ya kijiji pamoja na kupiga vita unyanyasaji kwa wananchi wa hali ya chini
Ataivyo amewaonya vijana kuendekeza pombe za kienyeji ambazo zimewafanya kulewa muda wote wa kazi na kuacha kufanya kazi za maendeleo na kujikuta wakishinda vijiweni na kushindwa kufanya kazi za kujingizia kipato na pia amesisitiza vijana kumtumikia mungu kwani kwa sasa katika maeneo mengi zilizopo nyumba za ibada wanaonekana wazee tu huku asilimia kubwa ya vijana wakikimbia misikiti na makanisa jambo ambalo ni kupoteza taifa lenye uwadilifu wa kumcha mungu
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Tanzania labour Part jimbo la vunjo Wilbard Moshi amesema wamempoteza mwanachama muhimu ambaye alikua amesha anza kazi ya kuhamasisha wananchi kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa kupata viongozi bora hivyo pengo lake ni vigumu kuliziba ila wanashukuru mungu kwa yote yalio tokea
Amesema chama hicho kitafanya jitiada za kumuenzi marehemu katika kufanya kazi kwa bidii kwa kumuunga mkono Mh Rais kwa lengo la wanachi wote kupata maendeleo ususani wananchi wa jimbo la vunjo pamoja ususani wananchi wa kata ya kahe ambapo marehemu alikua anawapigani kupata maendeleo ya araka zaidi ikiwemo ujenzi wa bara bara , zahanati masoko pamoja na kusimia miradi mbali mbali ya kijiji chao
Msiba huo uliudhuriwa na makada mbali mbali akiwemo Katibu wa Uwt Mkoa wa Kilimanjaro katibu wa mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa sasa James mbatia pamoja na waombolezaji kutoka Moshi mjini na vijijini