****************
NA EMMANUEL MBATILO
Kampuni ya Wasafi Media leo Juni 25 imezindua rasmi tamasha la Wasafi Festival 2019, ambalo linatarajiwa kufanyika katika mikoa nane nchini Bara na Visiwani.
Tamshama hilo linatarajiwa kufanyika kwa mara ya pili Julai 12 mjini Muleba kabla ya kuhamia Tabora Julai 14 mwaka huu, tangu kumalizika kwa tamasha la awali mwaka 2018.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mkurugenzi wa lebo ya WCB Wasafi ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz ametangaza rasmi kuanza kwa tamasha hilo kanda ya Ziwa mapema mwezi ujao.
Amesema licha ya kutangaza muziki huo kwenye mikoa ambayo itapata kushuhudia burudani hiyo amefafanua Zaidi katika kila mkoa utakaotembelewa itatolewa elimu kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
“Wasafi Festival licha ya kutoa burudani kwa jamii hatuachi hivhivi tofauti ilivyokuwa mwaka jana sehemu ya pili ya Tamasha hilo tunafanya bega kwa began a TACAIDS ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu hivyo tutapita vyuoni na kwenye konga mbalimbali za mikoa “. Amesema Diamond Platnumz.
Kwa upande wake Mratibu wa shughuli za Vijana TACAIDS, Bi. Grace Kessy amewataka wasanii pamoja na vijana ambao watahudhulia katika tamasha hilo kupokea elimu ambayo watawatia kuhusu matumizi bora ya Kondom ili kuweza kuwakinga vijana dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Hata hivyo kwa upande wa Afisa Sanaa kutoka BASATA, Bi. Bona Masenge amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wasanii wa WCB kwani mpaka sasa wanajitahidi kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na BASATA.