Home Mchanganyiko Baraza la Madiwani lalazimika kwenda kujifunza darasani Tunduma

Baraza la Madiwani lalazimika kwenda kujifunza darasani Tunduma

0

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakiwa pamoja na madiwani wa Halmashauri ya mji wa Tunduma kwenye ziara ya mafunzo ya kuona utekelezaji wa miradi ya elimu ya EP4R katika mji wa Tunduma.

Meya wa mji wa Tunduma Ally Mwafongo akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi hiyo mbele ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi

Meya wa mji wa Tunduma Mhe. Ally Mwafongo akisalimiana na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Elick Ambakisye( Mwenye koti jeusi) kwenye eneo la mradi

***************

Na Danny Tweve- Songwe

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbozi limefanya ziara kwenye miradi ya mpango wa EP4R  ili kuona namna Halmshauri ya mji wa Tunduma ilivyoweza kutekeza kwa ubora ndani ya muda mfupi .

Wilaya ya Mbozi ndiyo wilaya iliyofanikiwa kupewa kiasi kikubwa cha fedha nchini ikiongoza kwa kupewa zaidi ya 1.9 Bilion kutekeleza miradi ya shule 40 kwa kukamilisha majengo madarasa na vyoo  kwa shule zake kutokana na kufanikiwa katika vigezo vilivyowekwa ikiwemo watoto  uwiano wa kike wanaohitimu darasa la saba na kuingia sekondari bila kukwama

Vigezo vingine ni kuwahi kuingiza takwimu sahihi na kwa wakati za wanafunzi kwenye mfumo wa kuratibu sekta ya elimu nchini,  Kuwepo kwa uwiano wa vitabu na wanafunzi mashuleni kwa darasa la kwanza hadi la nne, Kurekebisha ikama ya walimu kwa kuhakikisha mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi kati ya 35 hadi 53 na kuwezesha watoto wanaosajiliwa Darasa la kwanza  wanamaliza darasa la saba kwa idadi ile ile, sambamba na shule za sekondari.

Kutokana na mafanikio hayo Halmashauri ya wilaya ya Mbozi imepokea kiasi hicho cha fedha kutekeleza miradi ya kukamilisha majengo ya shule za msingi, sekondari na vyoo kwa baadhi ya shule ambazo likuwa zimefikisha majengo yake kwenye hatua ya renta.

Hata hivyo kutokana na jitihada za wananchi, baadhi ya vijiji wameanzisha ujenzi wa majengo mapya kwa nguvu za wananchi ili fedha hizo zisaidie kukamilisha majengo hayo na hivyo kupunguza  na baadhi kumaliza kabisa upungufu wa vyumba vya kusomea pamoja na ofisi za walimu, huku jitihada zaidi zikielekezwa kwenye ujenzi wa vyoo.

Wilaya ya Mbozi kwa takwimu za mwaka 2018 kulingana  na Taarifa ya ukaguzi wa CAG, ina upungufu wa matundu ya vyoo 2427 kwa shule za msingi  ikilinganishwa na mahitaji ya matundu 4,467 na vyumba vya madarasa 1462 wakati mahitaji halisi ni 2306, upungufu wa   nyumba za walimu  696 kati ya mahitaji 1968.

Kwa upande wa shule za sekondari wilaya inakabiliwa na upungufu wa matundu 161 kati ya mahitaji ya matundu 527 huku kukiwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 38 kati ya mahitaji ya vyumba 527.