*****************
NJOMBE
Kikosi cha usalama barabarani cha jeshi la polisi mkoani Njombe kimeendesha zoezi la elimu kwa vitendo katika barabara kuu ya Njombe -Songea kwa watembea kwa mguu na madereva wa vyombo vya moto ili kukomesha kabisa tatizo la ajali za barabarani ambalo limetajwa na shirifa la afya duniani WHO kuwa linashika nafasi ya saba kwa kusababisha vifo duniani kote
Kwa mujibu wa WHO zaidi ya watu mil 1.3 hupoteza maisha kwa ajali za barabarani duniani huku katika mkoa wa Njombe takwimu zilizotolewa na kikosi cha usalama barabarani katika wiki ya usalama barabarani ilionesha takribani ajali 70 zilitokea na kusababisha vifo vya watu 74 na kuacha majeruhi 76 katika wilaya zote za nne za mkoa huo.
Kufuatia takwimu hizo kulitesa jeshi la polisi mkaoni humo kamanda wa kikosi cha usalama barabarani RTO Jenny Warioba anasema wamelazimika kutoa elimu hiyo kwa vitendo kwa watumia barabara kwa kuwa kumekuwa na uvunjifu mkubwa wa sheria za barabani jambo ambalo linasababishwa na uelewa mdogo wa sheria hizo na kutaja maeneo ya vivuko maarufu zebra kuwa ndiyo sehemu zenye uvunjifu mkubwa wa sheria .
Tobias Mkwabi na Devid Lyatuu ni baadhi ya madereva waliopatiwa elimu kwa vitendo katika vivuko vya mjini njombe wanaeleza itakavyosaidia kumaliza tatizo la ajali na kuomba jeshi hilo kuanza kutoa elimu hiyo mpaka mashuleni.
Kwa upande wa watembea kwa mguu akiwemo mzee Helmani Sanga nao wametoa maoni yao kuhusiana nae hatua hiyo ya jeshi la polisi kwa watumia barabara wanasema ni jambo jema huku wakiomba itolewe zaidi kwa umma kupitia majukwaa tofauti ili kuwajenge uelewa.
Jeshi linaendelea na elimu hiyo katika wilaya zote za mkoa wa Njombe ili kukomesha kabisa.