Kijana Bariki Josephat (aliyebeba begi) akiwa ameshikilia zawadi yake ya StarTimes Smart TV aliyopewa siku ya tamasha la Twenzetu kwa Yesu na wawakilishi kutoka StarTimes na viongozi wa dini.
Bariki Josephat alipokwenda kwenye ofisi za StarTimes kuchukua zawadi yake akiwa ameambatana na baba yake mzazi.
…………………….
Dar es Salaam.
Jumamosi iliyopita kulikuwa na tamasha la dini ambalo linajulikana kama ‘Twen’zetu kwa Yesu’ lililofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka likiwa na lengo la kukutanisha Vijana wa kikristo pamoja.
Mwaka huu StarTimes walikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na maelfu ya washiriki kutoka sehemu mbali mbali jijini Dar es Salaam.
Zaidi ya udhamini StarTimes walitoa zawadi mbalimbali kwa Vijana waliohudhuria tamasha hilo. Miongoni mwa zawadi hizo vilikuwemo ving’amuzi vitano vya Antenna vya StarTimes, Smart TV ya StarTimes inch 50 ambayo ilienda kwa kijana wa Usharika wa KKKT Mbezi jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahi sana kupata zawadi hii, kiukweli nilipokuwa nakuja kwenye tamasha la leo sikutegemea kama kutakuwa na kitu cha namna hii. Namshukuru sana Mungu pia nawashukuru StarTimes kwa zawadi hii.” Bariki Josephat, Mshindi wa Smart TV kwenye tamasha la Twen’zetu kwa Yesu.
Hata hivyo kijana Bariki baada ya kupokea zawadi hiyo yeye pamoja na ndugu zake waliomba kuiacha TV hiyo mikononi mwa StarTimes kwa sababu za kiusalama na kisha kufika kwenye ofisi zao siku ya Jumatatu kuichukua akiambatana na baba yake.
Mbali na tamasha hilo StarTimes wanaendelea kurusha michuano ya Copa America ambayo itaingia hatua ya robo fainali usiku wa kuamkia Ijumaa wiki hii kwa mechi kali ya Brazil vs Paraguay na Ijumaa usiku Venezuela vs Argentina. Zote kupitia chaneli za michezo za StarTimes kwa kiwango cha HD.