Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya Dkt Laizer wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali, uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Laizer akifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula (hayupo kwenye picha) pindi alipofungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma.
Sauti za Dkt Chaula, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, katika akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika jijini Dodoma
Baadhi Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakati alipofungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma.
Jopo la Wakuu wa Vyuo na Makaimu Wakuu wa vyuo vya Afya vya Serikali wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt Zainab Chaula wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa vyuo vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma.
…………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Zainab Chaula amefungua Mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya vya Serikali uliofanyika Jijini Dodoma.
Katika Mkutano huo Dkt. Zainab Chaula amewataka Wakuu wa vyuo kuongeza ubunifu katika utoaji huduma kwenye taasisi zao na kuboresha miundombinu jambo litakalosaidia kuinua kiwango cha elimu katika maeneo yao.
Kwa upande mwingine, Dkt. Chaula amewataka Wakuu hao wa vyuo vya Afya kuondoa dhana ya kuitegemea Serikali katika kila jambo ili kuwaletea Maendeleo, huku akisisitiza uanzishwaji wa vitega uchumi katika vyuo hivo jambo litalosaidia kupambana dhidi ya ukata wa fedha.
Aidha, Dkt Zainab Chaula amekemea vitendo vya uvunjaji wa maadili vinavyofanywa na baadhi ya Wakuu wa vyuo ikiwemo suala ya Rushwa, kufelisha wanafunzi, mambo yanayopelekea kutia doa Maendeleo ya taasisi hizo.
“Mkuu wa Chuo ni kama mzazi, kuna baadhi ya maeneo unakuta Mkuu wa chuo anatongoza wanafunzi, wengine wanafukuzisha wanafunzi, mnaharibu Watoto wa wenzenu, kwa hali hii tutazipata wapi baraka za Mwenyezi Mungu ” alisema Dkt Chaula
Mbali na hayo, Dkt Zainab amewapongeza Wakuu hao wa Vyuo kwa Juhudi wanazoendelea kuchukua katika kuboresha vyuo hivo licha ya changamoto lukuki wanazoendelea kukumbana nazo.
Dkt. Chaula aliendelea kusema kuwa, Serikali inatambua Juhudi kubwa zinazofanywa na Wakuu wa vyuo vya Afya nchini na kuahidi kupokea changamoto zote na kuendelea kutafutia ufumbuzi kadiri inavyowezekana.