Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw.Onesmo Olengurumwa akiongea na waadau mbalimbali walioweza kuhudhulia katika mkutano wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia Jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Bw.Ismail Suleimani akiongea na wadau mbalimbali walioweza kuhudhulia katika mkutano wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia Jijini Dar es Salaam leo.
Wadau mbalimbali wakiwa wanafuatilia mjadala katika mkutano wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia Jijini Dar es Salaam leo
********************
NA EMMANUEL MBATILO
Asasi za Kiraia wamekutana kwa pamoja kujadili mswada wa m,abadiliko ya sheria mbalimbali zinazoongoza Asasi hizo na baadae kufikisha kilio chao kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ili waweze kurekebisha vifungu ambavyo kama Muswada huo utapita kutakuwa na mazingira magumu ya utendaji kazi wa Asasi za Kiraia ikiwemo kufutwa kwa baadhi ya Asasi nchini.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika mkutano wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia kutoka katika sehemu mbalimbali, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw.Onesmo Olengurumwa amesema kuwa Tarehe 30 Mei mwaka 2019 serilaki iliwasilisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria mbalimbali katika nchi umezua sintofahamu na taharuki kwa AZAKI za ndani na nje ya nchi na huenda lengo lilikuwa kutokushirikisha AZAKi ambao ni walengwa wakuu kwenye Muswada huo.
“Tarehe 21 na 22 mwezi Juni 20o19 baadhi ya AZAKi ziliweza kuwasilisha maoni yetu mbele ya kamati za Bunge mjini Dodoma. Leo pia tumekutana hapa kwa dharura ili kujadili mapendekezo yetu na kuuhabarisha umma kuhusu Muswada huu. Umma unapaswa kujua kuwa Muswada huu ukipita hautaathiri AZAKi peke yake bali kila mtu ataathirika kwa kuwa AZAKi zipo kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii. kuleta maendeleo na ajira katika nyanja mbalimbali”. Amesema Bw.Olengurumwa.
Aidha Bw.Olengurumwa amesema kuwa kutokana na uchambuzi wa awali uliofanywa na Asasi za Kiraia zaidi ya 300 kuhusu Muswada huo ikiwa Muswada utapita kama ilivyo sasa utaleta changamoto nyingi katika utekelezaji wake na uendeshaji wa AZAKi nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Bw.Ismail Suleimani amesema kuwa baada ya kupitia Muswada huo wao wameona changamoto na madhara mengi yatatokea endapo Muswada huo utapita.
“Muswada huu ukipita utazitaka AZAKi zote zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni ambayo hayakuomba Hati ya kukubaliwa kufanya kazi kama mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya mwaka 2002 yatatakiwa kufanya kazi kama makampuni ya kibiashara kwa mujibu wa sheria ya makampuni na iwapo yatashindwa kufanya hivyo ndani ya muda wa miezi miwili yatafutiwa usajili bila ya kupewa taarifa”. Amesema Bw. Suleiman.