Baadhi ya wajane wakiwa katika maandamano ya kusheherekea Siku ya wajane Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenzwa na wajane wakati alipotembekea banda la Mtandao wa wajane Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia bidhaa za vikombe zinazotengenzwa na kikundi cha Maasai Market kutoka Kanda ya Kaskazini wakati alipotembekea banda lao katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wajane na wagane katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yalioyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu akielezea historia ya Siku ya Wajane Duniani wakati wa Maadhimisho ya Siku hiyo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa cheti kwa mwakilishi wa wajane Kanda ya Ziwa Bi. Rehema Said kwa kuwa moja ya mabanda matatu bora katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea bango lenye kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wajane Dunaiani kutoka kwa Mtandao wa Wajane Tanzania (TAWIA) katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wajane wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa aktika picha ya pamoja na wawakilishi wa wajane kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
…………………
Na ALEX SONNA, DODOMA.
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imezishauri halmashauri nchini kutenga asilimia nne kati ya 10 za mikopo inayotolewa na
Halmashauri hizo wapewe akinamama wajane ili waepukane
na mikopo yenye riba kubwa ambayo inachangia kuwarudisha nyuma
kimaendeleo.
Halmashauri hizo wapewe akinamama wajane ili waepukane
na mikopo yenye riba kubwa ambayo inachangia kuwarudisha nyuma
kimaendeleo.
Aidha imewataka wanawake ambao wana ndoa za asili wajitokeze
kwenda kufunga ndoa halali ili waweze kupata cheti cha kifo na cha
ndoa ambavyo vitawasaidia kudai urithi pindi watakapofiwa na waume zao.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa maazimisho ya siku ya wajane duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Naibu Waziri huyo,
amesema serikali imeamua kutoa agizo hilo ili kusaidia wakinamama
kuendesha maisha yao kupitia mikopo ya serikali ambayo ina unafuu.
Dkt. Ndugulile amesema kutokana na hilo anaziagiza halmashauri hizo
kupitia Wizara husika zifanye utaratibu wa kutoa elimu kwa kinamama
wajane katika mikoa mbalimbali jinsi ya kupata mikopo hiyo ambo ambalo
litachangia kupunguza ukali wa maisha baada ya kufiwa na waume zao.
Amesema kutokana na hilo anaziagiza halmashauri hizo kupitia Wizara
husika kuhakikisha wakinamama wanapewa elimu ya ukopaji ikiwemo kupewa
mikopo hiyo bila vikwazo vyovyote.
“kuanzia sasa hakuna sababu ya wajane hao kwenda kukopa mitaani wakati
serikali inatoa mikopo ambayo haina riba katika
halmshauri,kinachotakiwa kwa sasa ni asasi hizo kutoa elimu kwa wajane
ili wajue jinsi gani ya kupata mikopo hiyo,”amesema.
Kuhusu suala la wanawake kuwa na ndoa za asili
zisizotambulika, Dk. Ndugulile amesema wanatakiwa kwenda kufunga ndoa
halali ili waweze kupata cheti cha kifo,na cha ndoa ambavyo
vitawasaidia kudai urithi hapo baadae.
Amesema katika hilo pia asasi zisizo za kiserikali zinapaswa kuwapa
elimu wanawake hata kabla ya kupata matatazizo ya ujane juu ya kufunga ndoa halali ikiwemo kupata cheti cha ndoa ambacho kitakuwa kinga hapo baadae ya kumsaidia kupata na kile cha kifo ambavyo vyote kwa pamojavitakuwa ni vielelezo tosha vya yeye kupata haki yake ya msingi.
Kwa upande wake Katibu wa wizara hiyo Dkt. John Jingu amesema ofisi ya Takwimu inakadiria kuwa idadi ya wanawake wajane Tanzania ni 400,000 ambao ni sawa na asilimia 3.1 ya wanawake wote nchini ambao wanakadiriwa kuwa ni million 28.5 kwa mwaka 2019.
Amesema serikali inatambua kuwa wajane ni kundi muhimu
katika jamii hapa nchini,ndio maana wanaazimisha siku hiyo pamoja na
nchi nyingine duniani kote, ili kujua changamoto zinazowakabili wajane na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa kuzingatia sera ,miongozo sheria na kanuni mbalimbali za nchi yetu.
Maadhimisho hayo yanabebwa na kauli mbiu isemayo “Wezesha
Mafunzo ya Ujuzi kwa wajane ili kuchangia Malengo ya Maendeleo
Endelevu inapaswa kuzingatiwa ili kusaidia wakinamama wajane”.