**********************
NJOMBE
Mtoto Tunu Lukosi(10) mkazi wa Makambako Mkoani Njombe anaesoma darasa la sita mwenye kipawa cha kuimba nyimbo za injiri amefanya jambo la kustahajabu baada ya kutafuta fedha katika mazingira magumu ikiwemo huduma ya injiri na kuomba kwa waliofanikiwa na kisha kutoa msaada wa vyakula na mavazi katika kituo cha kulea watoto yatima wenye umri chini ya miaka miwili na wale waliotupwa na wazazi wao .
Akifafanua sababu ya kuguswa na kulazimika kutafuta fedha katika za misaada hiyo ya kibinadamu mtoto Katika kituo cha Yatima Ilembula Tunu anasema yatima wengi wamekuwa wakiishi nje ya matarajio yao kwa kuishi katika mazingira magumu hivyo kwa kuwa mungu amemtunuku kipawa atakitumia kuwasaidia wenye uhitaji huku akitoa rai kwa jamii na watoto wengine kuwasaidia yatima kote duniani huku mama mzazi Neema Sanga akieleza jinsi mwanae alivyokubali kusimama shule ili atafute fedha ya kusaudia yatima .
Nae Silvia Anania mlezi wa watoto na Regina Joseph afisa ustawi Ilembula hospitali wakiongelea changamoto zinakikabili kituo hicho cha kulea watoto yatima wanasema ni ukata wa fedha za uendeshaji kwa kuwa hakina ufadhili wa namna yeyote jambo ambalo limfanya afisa ustawi kutoa rai kwa umma kuhusu athari za watoto kukulia kwenye vituo yatima huku akiwataka kupelekwa vituo humo watoto ambao wamekosa kabisa usadizi kwa kuwa watoto wanahitaji upendo wa ndugu na majirani.
Kituo cha Ilembula cha kulea watoto yatima kilianzisha na hospitali ya Ilembula miaka 1963 kwa lengo la kunusuru maisha ya watoto wakipoteza wazazi wao wakati wa kujifungua , mikasa ambayo ilikuwa ni mingi pamoja na waliokuwa wakiokotwa na kueleza jinsi kituo hicho kilivyo tengeneza njia kwa watoto wengi na kuomba msaada kwa watu wengine wenye uwezo.
Miongoni mwa watu walioguswa na kitendo cha mtoto Tunu kusimamia msimamo wake wakutafuta fedha ili kuwasaidia yatima ni pamoja na mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Edward Mwalongo , mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa ndugu na majirani wa familia ya tunu.