*********************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
MASHINDANO ya kugombea kombe linaloandaliwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya CCM, Rita Kabati yanayojulikana kwa jina la ‘Kabati Challenge Cup 2019’ yamezinduliwa rasmi kwa kuzikutanisha timu za Kitwiru Fc na Black Eagle katika mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya Msingi Ipogoro.
Katika mchezo huo ambao uliingia dosari katika dk ya 90 baada ya mashabiki wa Black Eagle kuingia uwanjani kugomea goli la tatu lilofungwa kwa njia ya penati na timu ya soka ya Kitwiru hali iliyolazimika refa wa mchezo huo kumaliza na kupewa ushindi timu ya Kitwiru na Black Eagle kuondolewa rasmi katika mashindano hayo yanayofanyika kwa njia ya mtoano.
Katika mchezo huo magoli ya Kitwiru mawili yalifungwa na Joseph Mlua dk. 6 na dk 50 na goli la tatu lilifungwa na George Luvanda katika dk 90 huku magoli ya Black Eagle yalifungwa na Jackson Mhavile dk 25 na Bony Kilave wa Kitwiru alijifunga katika dk. 75. na kuipatia timu ya soka ya Black Eagle goli la pili.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, Mwenyekiti wa mashindano hayo, Gerald Malekela alisema kuwa jumla ya 44 za mkoani Iringa zitashiriki mashindano ya Ritta Kabati Challenge awamu ya tatu 2019 katika viwanja mbalimbali ya mpira wa miguu mkoani Iringa kwa kuzishilikisha timu za wilata ya Iringa, Iringa vijijini na Mufindi.
“Kwa mara ya kwanza tumepata timu nyingi kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini kwa kujitokeza timu kumi na moja hiyo inaonyesha jinsi gani kila kukicha mashindano haya yanazidi kuwa na mvuto na ushindani unaongezeka” alisema Malekela
Malekela alisema msimu huu mashindano yatakuwa bora kuliko misimu iliyopita kwa kuwa kamati imejipanga kuhakikisha wanatengeneza kitu kilicho bora na kuongeza thamani ya mashindano na kuweka alama ya kuigwa kwa wapenda michezo hasa mchezo huu wa mpira wa miguu.
Malekela aliongeza kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani wa Iringa, lakini pia kutengeneza ajira kwao, sambamba na kutengeneza kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.
Aidha alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto ya ubovu na uhaba wa viwanja vya mpira wa miguu,hivyo tunaiomba serikali kuhakikisha wanatusaidia kuboresha viwanja hivyo.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Iringa,(IRFA) Dk. Ally Ngala alisema kuwa kuwa mbunge huyo ameonyesha jitihada kubwa katika kuendeleza soka mjini Iringa na kumuomba kuendelea zaidi kusaidia soka Iringa.
Ngala alisema mashindano hayo yameleta chachu kubwa ya soka katika mkoa wa Iringa ambapo vijana wengi wamehamasika na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika soka na kuwa lazima kuweka mkakati wa kudumu wa kuendeleza vijana hao kisoka