Baadhi ya waumini wakibariki ndoa zao na kuwekewa mikono ya baraka na Askofu Mstaafu Dr.Israel Mwakyolile kwenye ibada ya leo katika kanisa la KKT Vwawa Wilayani Mbozi.
Aliyekuwa Meneja wa TRA mKOA WA Songwe Bw.Paul Walalaze ambaye amehamishiwa mkoa wa TRA wa Temeke kuwa Meneja akiwekewa mikono ya baraka na Askofu Mstaafu Dr.Israel Mwakyolile mara baada ya kuwaaga waumini wenzakw kwenye ibada hiyo.
…………………
Na Danny Tweve Songwe.
Askofu Mstaafu wa KKKT –Dayosisi ya Konde Dr Israel Mwakyolile amesema, katika mazingira ya sasa ni lazima wa Tanzania waendelee kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kundi dogo la waathirika wa mirija michafu iliyokuwa inapitisha hewa ya watanzania wengi kuanza kutafuta namna ya kujinasua hata kwa kutumia mbinu chafu.
Akizungumza kwenye ibada ya kutimiza miaka 33 kwa Kanisa la KKKT Usharika wa Vwawa, Makao makuu ya Mkoa wa Songwe, Askofu Mwakyolile amesema ni muhimu kuliko wakati mwingine kwa Watanzania kumwombea Rais wao kwa yale anayoyasimamia.
Amesema katika kipindi hiki, kuna watu wanapata tabu sana kutokana na mtazamo wa serikali ambapo fulsa kwa wanyonge zimekuwa zikifunguliwa huku wachache walafi wakibanwa, hivyo wapo wanaotafuta njia chafu za kuzima jitihada hizo jambo ambalo watanzania wanapaswa kufanya maombi kwa kadiri wawezavyo.
Katika ibada hiyo aliyekuwa meneja wa TRA mkoa wa Songwe Paul Walalaze aliwekewa mikono ya Baraka yeye na mkewe wakati wa kuaga, kufuatia kuhamishiwa Mkoa wa Temeke huku akiwa ameupandisha mkoa wa Songwe katika makusanyo ya mamlaka ya Mapato kwa mwaka wa pili mfululizo.
Aidha katika ibada hiyo zaidi ya waumini 50 walibariki ndoa zao katika ibada hiyo kutokana na utaratibu wa Kiongozi wa Usharika mchungaji John Mwasakilali kutenga siku ya maadhimisho ya kanisa kuwa sehemu pia ya kuunganisha ndoa za waumini wake, zoezi ambalo limepokewa pia na watu waliofikisha umri wa miaka 60 kwenye ndoa zao kupata Baraka.