Baadhi ya watumishi wakihamisha matofali kwenda katika jengo la wazazi linaloendelea kujengwa
Katikati Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Omary Sukari akinyanyua tofali kwa ajili ya ujenzi unaoendelea wa hospitali ya wilaya ya Tanganyika, kulia kwake ni Afisa Utumishi Mkoa wa katavi Bi. Cresensia Joseph
Baadhi ya watumishi wakifanya usafi kwa kufyeka nyasi katika eneo la hospitali ya wilaya ya Tanganyika
Jengo la maabara likiwa tayari limekwishaezekwa
****************
22.06.2019
Na Mwandishi Wetu Katavi
WATUMISHI WA SEKRETARIATI YA MKOA WA KATAVI WAJITOKEZA KUJENGA HOSPITALI
Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma watumishi wa sekretariati ya mkoa wa katavi wamejumuika na mafundi katika kusaidia kazi mbalimbali za ujenzi katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika lengo likiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Afisa Utumishi wa Mkoa Bi. Cresensia Joseph amesema lengo la zoezi hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali kutoa huduma kwa wananchi
Amesema watumishi wanatambua azma ya serikali ya kufikisha huduma karibu na jamii hivyo nao wamejitoa kwa nguvu zao kushiriki katika ujenzi huo
Aidha baadhi ya watumishi walioshiriki katika zoezi hilo wamesema wanafanya hivyo katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusogeza huduma za afya kwa jamii
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dkt. Selemani Mtenjela amesema hospitali hiyo ikikamilika itahudumia zaidi wakazi laki tatu wa wilaya hiyo
Ameongeza kuwa hospitali hiyo ikikamilika itawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 130 wakazi wa wilaya hiyo kufuata huduma za afya katika hospitali ya manispaa ya Mpanda