Huo ukawa ndiyo mwanzo wa safari ya kujionea maajabu ya Rais Dk.John Magufuli katika Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa, ambapo katika bandari ya Mwanza Kusini nikaona ujenzi wa eneo kubwa la Chelezo kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria na meli ya MV Victoria ikikarabatiwa.
Meli ya Mv Clarias inayofanya safari kati ya Ukerewe na Mwanza pamoja na visiwa vya ziwa Victoria chini ya usimamizi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).
………………………………
Basi siku hiyo Tukalala, siku iliyofuata ilikuwa Juni 3 tuliamka mapema kujiandaa kwa ajii ya kuanza kazi rasmi. Ratiba ya siku hiyo ilikuwa kwenda kushuhudia Meli ya Mv Clarias inayotia nanga katika Bandari ya Mwanza Kaskazini kupakia abiria wa Nansio Ukerewe na maeneo mengine ya viswani vya ziwa Victoria kisha inarudi tena Mwanza.
Kwa sababu dereva wetu Hassan Shaban alikuwa amelala mbali na Logde tuliyolala sisi ilibidi asubuhi ile tumsubiri ili aje kutuchukua. lakini kidogo alichelewa labda kwa sababu ya uchovu, muda wa meli kuondoka ulikuwa unayoyoma manake ilikuwa inaondoka saa tatu hivi za asubuhi.
Basi nilipoona Dereva kachelewa na kuna dalili za kushindwa kufanya kazi hiyo nikafanya maamuzi nikaita Pikipiki (Bodaboda) na kuondoka haraka kwenda Bandari ya Mwanza Kaskazini, nilipofika nikaripoti Kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya bandari Mwanza Bw. Geofrey Lwesya ambaye alinipa mfamyakazi mmoja aliyetakiwa kunipeleka kwenye meli.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya bandari Mwanza Bw. Geofrey Lwesya akitoa ufafanuazi wa mambo kadhaa kwa waandishi waliotembelea katika bandari ya Mwanza Kusini hivi karibuni
…………………………………………
Tuliposhuka chini kutoka ofisini nilikuta tayari na waandishi wenzangu hasa wapiga picha wameshafika kwa kutumia usafiri wa pikipiki (Bodaboda) pia Kisha tukaanza kazi ya kupiga picha mbalimbali wakati abiria wakipanda kwenye Meli ya Mv Clarias na kufanya nao mahojiano baadaye meli iliondoka kuelekea Nansio Ukerewe.
Niliamua kuchukua usafiri wa Pikipiki kutoka Lodge kwa sababu sikutaka kukwama au kukwamisha kazi ya watu walionituma kwa sababu bila kufanya vile muda ulikuwa unaondoka na nisingeweza kupata picha za ile meli wakati inapakia abiria na kuondoka bandarini.
Hivyo niliona nisimamie lengo langu mpaka litimie nisikubali kukwamishwa kubwa zaidi lilikuwa ni kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa.
Baadaye dereva Hassan Shaban alikuja na Kijana Humprey Shao aka (Mtu wa Story) Bandari ya Mwanza Kaskazini wakatuchukua mpaka kwenye hoteli ya siku nyingi jijini Mwanza inayomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara Mh. Lameck Airo inayoitwa Lakairo.
Hapo waandishi wote tuliokuwa katika ziara ile tuliandaliwa supu baabkubwa ya samaki sato na ndizi, Supu hiyo iliandaliwa na mmoja wa waratibu wa ziara yetu jina kapuni tukajichana vya kutosha matumbo yakawa ndiii tukaendelea kushushia na chupa za maji tu.
Utayarishaji wa eneo la ujenzi wa Chelezo kitakachotumiwa na wakandarasi wa ujenzi wa meli mpya katika Bandari ya Mwanza Kusini ukiendelea .
………………………………………..
Baada ya hapo mida ya mchana tulienda katika bandari ya Mwanza kusini hapa kunatekelezwa miradi minne mikubwa ambayo ni Chelezo kwa ajili ya kujenga meli mpya ya abiria, Ujenzi wa Meli yenyewe na Ukarabati wa Meli za MV Victoria na MV Butiama unaosimamiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).
Miradi hii kwangu niliona maajabu kwa sababu yote inatekelezwa kwa wakati mmoja na nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe kazi ikiendelea katika bandari ya Mwanza Kusini.
Kwa mujibu wa Mendaji Mkuu wa MSCL Bw. Eric Hamissi mradi wa ujenzi wa Chelezo katika bandari ya Mwanza Kusini unagharimu kiasi cha dola za kimarekani Milioni 15,814,747 mradi huo unajengwa na kampuni ya M/S STX ENGINE CO.LTD kwa kushirikiana na kampuni ya SAEKYUNG Construction Company Limited na umepangwa kukamilika mwezi Desemba 2019.
Eric Hamissi anaongeza kuwa mradi wa pili ni Ujenzi wa Meli mpya itakayofanya kazi katika Ziwa Victoria ambao unagharimu dola za Kimarekani milioni 39,000,000.00, Meli hii inajengwa na kampuni ya M/S GAS ENTEC Co Ltd kwa kushirikiana na kampuni ya Kang Nam Corporation na SUMA JKT na mradi unatarajiwa kukamilika Sepemba 2020.
Meli ya MV Victoria ambayo ipo kwenye ukarabati mkubwa.
…………………………………………………
Mtendaji Mkuu huyo ameongeza kuwa mradi wa tatu ni Ukarabati wa meli ya MV. VICTORIA inayofanya kazi katika Ziwa Victoria unaogharimu shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni 22.7 mradi huu unatekelezwa na kampuni ya M/S KTMI kwa kushirikiana na kampuni ya Yuko’s Enterprises A.E Limited utaokamilika Machi 2020.
Anamazilia kwa kusema mradi wa nne ni wa Ukarabati wa meli ya MV. Butiama inayofanya kazi pia katika ziwa Victoria huu unagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni 4. 8 na unatekelezwa na kampuni ya M/S KTMI kwa kushirikiana na kampuni ya Yukos Enterprises E.A Limited huu utakamika February 2020 utekelezaji wa miradi yote hii unakwenda pamoja.
Mendaji Mkuu wa Shirika la huduma za meli (MSCL) Bw. Eric Hamissi.
…………………………………………..
Kwangu mie baada ya kushuhudia haya niliyoyaona pale bandari ya Mwanza Kusini, niliona ni maajabu ya utekelezaji wa miradi ya serikali chini ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mzalendo Dkt. John Pombe Magufuli utekelezaji unaokwenda kwa kasi ya ajabu kabisa.
Baada ya kazi siku hii nayo ikaisha nikarudi hotelini pamoja na wenzangu ili kumalizia kazi za siku hiyo na kujiandaa na safari ya Musoma mkoani mara juni 4 ili kuona nini kinaendelea kuhusu wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya bandari katika maziwa makuu nchini………………….
.INAENDELEA
ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII NITAKUSIMULIA MWANZO MWISHO MAAJABU YA RAIS MAGUFULI NILIYOYAONA.