Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa,akisoma taarifa kwa Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakati akifungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Winifrida Kaliyo,akizungumza na wasomi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakati alipofungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
Baadhi ya wasomi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakati akifungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akipokea Taarifa kutoka kwa Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa kabla ya kufungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda,akizungumza na wasomi nchi wakati wa kufungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameweka mambo muhimu tano ya kuzingatia kwa wasomi wa vyuo vikuu yatakuwa msaada kwao kuelekea zuala nzima la ukosefu wa ajira nchini.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma.
Mhe.Pinda amewaambia kuwa serikali haiwezi kuwaajiri vijana wote wanaohitimu elimu ya juu hivyo amewataka wawe na njia ya pili ambayo itawapa mtaji.
“Nchi haiwezi kuajiri wasomi wote ili niliweke wazi hivyo tulipaswa kutengeneza mfumo ambao utawafanya wahitimu kuwa na muelekeo wa kutumia fursa zilizopo”amesema Mhe.Pinda
Mhe.Pinda ametaja jambo la kwanza ni kuwepo kwa mfumo wa elimu utakaowawezesha kupata elimu ya ujasiliamali katika kila ngazi ya masomo wanayoifikia.
“Kama mwaka wa kwanza hadi mwaka wa tatu kwenye masomo yake akapatiwa mbinu mbalimbali zitakazomuwezesha kubaini fursa za ujasiliamali zilizopo, kwa kiasi kikubwa tutaweza kukabiliana na ukosefu wa ajira”aamesema Pinda
jambo la pili amewataka wasomi kuzingatia ni kubadili mtizamo wa kifikra kwamba pindi watakapo hitimu masomo wataajiriwa.
Aidha amesema kuwa alifanya ziara ya kuongea na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo mmoja wa wasomi wa masomo ya sheria,alimueleza jinsi alivyopata tabu pindi alipoambiwa afuge kuku, wakati amejifunza masuala ya sheria.
Jambo la tatu ambayo wanafunzi hao ni muhimu kuzingatia ni kufahamu uhalisia wa dunia ya sasa.
“Itawalazimu mshindane na watu kutoka mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) au maeneo mengine duniani”amesisitiza
Pinda ametaja jambo la nne ambalo ni uthubutu katika kufanya maamuzi.
Amesema kuwa baadhi ya wasomi wa vyuo vikuu wamekuwa na desturi ya kuwakatisha tamaa wenzao ambao wana mawazo ya kujiajiri.
Mhe.Pinda amemalizia jambo la tano ambalo amewaeleza wanafunzi hao ni kufahamu tofauti waliyokuwa nayo na wale ambao hawakupata fursa ya kusoma elimu ya juu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Winifrida Kaliyo, amesema kuwa semina hiyo imelenga kuwawezesha wanafunzi kutambua fursa kisha kuzitumia kiuchumi.
Awali Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa, amesema kuwa tangu Januari hadi Juni mwaka huu, umoja huo umeongeza wanachama wapya 1500.
Aidha,amesema kuwa wametoa mafunzo kwa viongozi ngazi ya kata hadi wilaya pamoja na kuhamasisha wanawake kugombea ngazi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.